Niliifanya kwa mwezi mmoja nimerudisha mashine maana faida kiduchu sana...
Kwa siku kuna mtu alikuwa ananipa hadi 30m nimuwekee sasa hapo lazima mtu aende bank aweke mzigo alafu utume kwa huyo mtu....nilipambana mwa mwezi mmoja na kwa siku chini kabisa nilikuwa natuka 5m.mwisho wa mwezi nikapokea 155,000 [emoji16][emoji16].
Nikaizima siku hiyo hiyo maana mtu amaweza kukupa hela ukaenda bank wakasomea ramani ikala kwako.
Nmb ndo wanasema ina commision nzuri.
Hii kazi ukiifanya kama agent uwe na kazi ya miamala tu labda ndo utapata commision kubwa.
Gharama ya machine ni 270,000.
Hapo nimeshairudisha nimekula hasara hiyo niliona kwangu ni biashara kichaa....kazi ya hela ni ngumu sana hapo bado hujaibiwa, kukosema miamala, majambazi nk
Sent using
Jamii Forums mobile app