Naomba kujua dalili za kisukari maana nahangaika

Naomba kujua dalili za kisukari maana nahangaika

pua200
1. Kunywa maji mara kwa mara (kiu ya mara kwa mara)
2. Kukojoa mara kwa mara (mkojo mweupe peer)
3. Kupungua uzito kwa kasi Sana.
 
Hivi huna Dada wewe? Anatafuta au anatafutwa.
Wakenya bana
Ni kweli madada wanatafutwa, lakini mpaka umejua kupiga Dompo kweli ?!. Mabinti wanaotafutwa hawapo kwenye chama la Dompo mamii [emoji12][emoji23][emoji1787].

Nashauri tu, usichague sana na kama kuna kachanga jisalimishe.

Umezungumzia Kenya , plz inahusiana nini mada hii ya Diabetic . Kama ni jina tunazo wilaya mbili labda mwambieni no. 1 azigawe kwa Kenyatta kama atakuelewa [emoji40][emoji850].
 
Ni vizuri kwenda hospitali kufanya kipimo cha damu kinachoitwa HbA1c. Hiki kipimo kitakupa wastani wa kiwango cha sukari kwenye damu yako kwa miezi mitatu iliopita. Matokeo yakiwa 5.6 na chini huko poa, 6 kwenda juu una kisukari. 5.7 - 5.9 ugonjwa wa kisukari uko njiani.

Uziru wake kama umepata kisukari ukubwani, yani Type 2 diabetes , unaweza kuutokomeza ugonjwa kwa mambo ya kawaida tu kama kufanya mazoezi au kuangalia vitu unavyokula na mda unao kula.

Kuna ugonjwa wa kisukari wa kuzaliwa nao, yani Type 1 diabetes, huu hautibiki bali utakuwa unatumia insulin na pia kuangalia kiwango chako cha sukari kila siku hili uweze kumudu kiwango cha sukari mwilini mwako.

Turudi kwenye swali lako, dalili za kisukari. Sasa sukari inaposhuka san mwilini ni hatari zaidi kuliko sukari inapokuwa juu.

Sukari inapokuwa chini mtu unajisikia uchovu, joto kali, kizunguzungu na inaweza kushuka mpaka unashindwa kuona na unatetemeka mpaka unapoteza fahamu na kufariki kama ujapata uduma ya kwanza kwa mda muafaka. Mara nyingi wagonjwa wa kisukari wanashauriwa kutembea jabo na pipi mfukoni, kwani sukari ikianza kushuka na unahisi hizi dalili, kama hamna chakula karibu utamumunya pipi hili sukari yako ipande juu kukupa mda wa kutafuta chakula haraka sana. Mtu mwenye tabia za sukari kushuka kabla ya kulala ni vizuri akapata mlo mdogo kama karanga za kusaga na mkate kwani ni vibaya mno sukari ikishuka sana wakati unaamka au umelala.

Sukari inapokuwa juu, unakuwa unakojoa mara kwa mara, na unasikia kiu sana, uchovu na kukosa kuona vizuri. Mara chache sana ufika juu mpaka upate dalili hizi kwani mara nyingi huwa kabla a kula wanaangalia kiwango cha sukari na kuchoma sindano ya insulin kutokana na matokeo ya kiwango cha sukari. Insulin inasaidia kushusha sukari chini na unapochoma sindano kabla ya kula itabalance kiwango cha sukari. Mara nyingi kama kiwango cha sukari ni chini ya 200 ml/dL basi huitaji kuchoma sindano kabla ya kula, lakini kama ni juu unaitaji kuchoma sindano hili ukila chakula sukari yako hisipande juu zaidi. Pia kuna vidonge vya kuweza kumudu sukari yako , kila mtu tofauti na ni daktari ndie anaweza kukusaidia kujua hipi inakufaa. Kuna insulin ambazo zinamudu sukari kwa mda mrefu, yani ukichoma inakaa mwilini mwako kwa mda mrefu na kuna ambayo ukichoma tu, lazima ule chakula au sukari yako itashuka sana (hii ndio nimezungumzia hapo ju unachoma kutokana na kiwangu chako cha sukari).

Sasa kwa nyumbani kwa vile maisha ni magumu na sio wote wanaweza kumudu gharama za kuangalia sukari kila siku, ni vizuri kwanza kufanya japo kipimo hili ukishajua ujaribu kumudu ugonjwa kwa njia ya chakula na mazoezi. Na ukiona mtu mwenye dalili za sukari kushuka sana basi mpe juisi au pipi kuokoa maisha yake kama anafahamu bado na kuweza kumeza. Usijaribu kumpa kitu chochote mdomoni kama hajitambui kwani unaweza kuleta matatizo zaidi, mpeleke kwenye hospitali ya karibu mara nyingi kuna sindano wanaweza kumchoma kufanya sukari yake ipande. Kutaka kujua kama mgonjwa wako ana uwezo wa kujitambua kidogo kabla kumpa kitu mdomoni muulize maswali madogo rahisi kama jina lake, jina la rais, au leo siku gani.
 
Hangover hiyo.
Kuitibu kuna mawili, zimua mvinyo tena au tumia painkillers na unywe maji kwa kwingi na vile vile pumzika.
 
Ni vizuri kwenda hospitali kufanya kipimo cha damu kinachoitwa HbA1c. Hiki kipimo kitakupa wastani wa kiwango cha sukari kwenye damu yako kwa miezi mitatu iliopita. Matokeo yakiwa 5.6 na chini huko poa, 6 kwenda juu una kisukari. 5.7 - 5.9 ugonjwa wa kisukari uko njiani.

Uziru wake kama upemata kisukari ukubwani, yani Type 2 diabetes , unaweza kuutokomeza ugonjwa kwa mambo ya kawaida tu kama kufanya mazoezi au kuangalia vitu unavyokula na mda unao kula.

Kuna ugonjwa wa kisukari wa kuzaliwa nao, yani Type 1 diabetes, huu hautibiki bali utakuwa unatumia insulin na pia kuangalia kiwango chako cha sukari kila siku hili huweze kumudu kiwa cha sukari mwilini mwako.

Turudi kwenye swali lako, dalili za kisukari. Sasa sukari inaposhuka mwili ni hatari zaidi kuliko sukari inapokuwa juu.

Sukari inapokuwa chini mtu unajisikia uchovu, joto kali, kizunguzungu na inaweza kushuka mpaka unashindwa kuona na unatetemeka mpaka unapoteza fahamu na kufariki kama ujapata uduma ya kwanza kwa mda muafaka. Mara nyingi wagonjwa wa kisukari wanashauriwa kutembea jabo na pipi mfukoni, kwani sukari ikianza kushuka na unahisi hizi dalili, kama hamna chakula karibu utamumunya pipi hili sukari yako ipande juu kukupa mda wa kutafuta chakula haraka sana. Mtu mwenye tabia za sukari kushuka kabla ya kulala nivizuri akapata mlo mdogo kama karanga za kusaga na mkate kwani ni vibaya mno sukari ikishuka sana wakati unaamka au umelala.

Sukari inapokuwa juu, unakuwa unakojoa mara kwa mara, na unasikia kiu sana, uchovu na kukosa kuona vizuri. Mara chache sana ufika juu mpaka upate dalili hizi kwani mara nyingi huwa kabla a kula wanangalia kiwango cha sukari na kuchoma sindano ya insulin kutoka na matokeo ya kiwango cha sukari. Insulin inasaidia kushusha sukari chini na unapochoma sindano kabla ya kula itabalance kiwango cha sukari. Mara nyingi kama kiwango cha sukari ni chini ya 200 ml/dL basi huitaji kuchoma sindano kabla ya kula, lakini kama ni juu unaitaji kuchoma sindano hili ukila chakula sukari yako hisipande juu zaidi. Pia kuna vidonge vya kuweza kumudu sukari yako , kila mtu tofauti na ni daktari ndie anaweza kukusaidia kujua hipi inakufaa. Kuna insulin ambazo zinamudu sukari kwa mda mrefu, yani ukichoma inakaa mwilini kwako kwa mda mrefu na kuna ambayo ukichoma tu, lazima ule chakula au sukari yako itashuka sana (hii ndio nimezungumzia hapo ju unachoma kutokana na kiwangu chako cha sukari).

Sasa kwa nyumbani kwa vile maisha ni magumu na sio wote wanaweza kumudu gharama za kuangalia sukuri kila siku, ni vizuri kwanza kufanya japo kipimo kwanza hili ukishajua ujaribu kumudu ugonjwa kwa njia ya chakula na mazoezi. Na ukiona mtu mwenye dalili za sukari kushuka sana basi mpe juisi au pipi kuokoa maisha yake kama anafahamu bado na kuweza kumeza. Usijaribu kumpa kitu chochote mdomoni kama hajitambui kwani unaweza juleta matatizo zaidi, mpeleke kwenye hospitali ya karibu mara nyingi kuna sindano wanaweza kumchoma kufanya sukari yake ipande. Kutaka kujua kama mgonjwa wako ana uwezo wa kujitambua kidogo kabla kumpa kitu mdomoni muulize maswali madogo rahisi kama jina lake, jina la rais, au leo siku gani.
Yaani wewe umekuja palepale, huwa nakosa nguvu na natetemeka, mpaka nahisi kupatiwa kitu Cha kula ndiyo nirejee katika hali ya kawaida. Inanitokea nikiamka nikala kauichai na muhogo, siku hiyo nisipokula haraka natetemeka, otherwise nikiamka nikala kasupu, chai na wali chapati, nakuwa sawa sawa. Tatizo ni sukar au kula la ziada
 
Kuna mtu "atapigwa" hapa. My inner voice inaniambia mleta mada ni mvulana
 
Nenda kapate vipimo sahihi Hospitali achana Na Makanjanja wa humu

Humu JF Hata ukiuliza hatua Za kutengeneza BOmu la Nyuklia utawapata Washauri wanaojifanya Na wana uzoefu wa kutosha

Kumbe wa huko hospitalini hawamo humu!
 
Nenda kapate vipimo sahihi Hospitali achana Na Makanjanja wa humu

Humu JF Hata ukiuliza hatua Za kutengeneza BOmu la Nyuklia utawapata Washauri wanaojifanya Na wana uzoefu wa kutosha

Kumbe wa huko hospitalini hawamo humu!
 
Yaani wewe umekuja palepale, huwa nakosa nguvu na natetemeka, mpaka nahisi kupatiwa kitu Cha kula ndiyo nirejee katika hali ya kawaida. Inanitokea nikiamka nikala kauichai na muhogo, siku hiyo nisipokula haraka natetemeka, otherwise nikiamka nikala kasupu, chai na wali chapati, nakuwa sawa sawa. Tatizo ni sukar au kula la ziada

Kwanza kafanye kipimo cha damu kujua kama ugonjwa unao au la.

Pili jaribu kula kwa mda maalum, bila ya kuchelewa.

Tatu kula kitu kidogo kama karanga, korosho, biskuti kati kati ya milo yako mikuu. Itasaidia kuzuia sukari yako kushuka wakati unafanya shughuli zako sana sana kazini.
 
Sijasoma comments zote, lakini naamini ushapewa dalili zote, ninachoongezea, type 2 diabetes, mara nyingi(nimesema mara nyingi) huanzia age ya 40. Na wewe hujafika. Its better kupima mapema, hasa kama kipo kwenye ukoo wenu, ili uanze ku-control kwa chakula.
++++Merry Christmas, nimeshiba vinono hadi nimesahau kuwa leo ni jumanne, na huko nje kitaa vyuma vimekaza!! Hata nimesahau kuwa uchaguzi ujao utasimamiwa na tume mpya kutoka kile chuo pale Moshi. Hello tz!!
 
Back
Top Bottom