Ni vizuri kwenda hospitali kufanya kipimo cha damu kinachoitwa HbA1c. Hiki kipimo kitakupa wastani wa kiwango cha sukari kwenye damu yako kwa miezi mitatu iliopita. Matokeo yakiwa 5.6 na chini huko poa, 6 kwenda juu una kisukari. 5.7 - 5.9 ugonjwa wa kisukari uko njiani.
Uziru wake kama upemata kisukari ukubwani, yani Type 2 diabetes , unaweza kuutokomeza ugonjwa kwa mambo ya kawaida tu kama kufanya mazoezi au kuangalia vitu unavyokula na mda unao kula.
Kuna ugonjwa wa kisukari wa kuzaliwa nao, yani Type 1 diabetes, huu hautibiki bali utakuwa unatumia insulin na pia kuangalia kiwango chako cha sukari kila siku hili huweze kumudu kiwa cha sukari mwilini mwako.
Turudi kwenye swali lako, dalili za kisukari. Sasa sukari inaposhuka mwili ni hatari zaidi kuliko sukari inapokuwa juu.
Sukari inapokuwa chini mtu unajisikia uchovu, joto kali, kizunguzungu na inaweza kushuka mpaka unashindwa kuona na unatetemeka mpaka unapoteza fahamu na kufariki kama ujapata uduma ya kwanza kwa mda muafaka. Mara nyingi wagonjwa wa kisukari wanashauriwa kutembea jabo na pipi mfukoni, kwani sukari ikianza kushuka na unahisi hizi dalili, kama hamna chakula karibu utamumunya pipi hili sukari yako ipande juu kukupa mda wa kutafuta chakula haraka sana. Mtu mwenye tabia za sukari kushuka kabla ya kulala nivizuri akapata mlo mdogo kama karanga za kusaga na mkate kwani ni vibaya mno sukari ikishuka sana wakati unaamka au umelala.
Sukari inapokuwa juu, unakuwa unakojoa mara kwa mara, na unasikia kiu sana, uchovu na kukosa kuona vizuri. Mara chache sana ufika juu mpaka upate dalili hizi kwani mara nyingi huwa kabla a kula wanangalia kiwango cha sukari na kuchoma sindano ya insulin kutoka na matokeo ya kiwango cha sukari. Insulin inasaidia kushusha sukari chini na unapochoma sindano kabla ya kula itabalance kiwango cha sukari. Mara nyingi kama kiwango cha sukari ni chini ya 200 ml/dL basi huitaji kuchoma sindano kabla ya kula, lakini kama ni juu unaitaji kuchoma sindano hili ukila chakula sukari yako hisipande juu zaidi. Pia kuna vidonge vya kuweza kumudu sukari yako , kila mtu tofauti na ni daktari ndie anaweza kukusaidia kujua hipi inakufaa. Kuna insulin ambazo zinamudu sukari kwa mda mrefu, yani ukichoma inakaa mwilini kwako kwa mda mrefu na kuna ambayo ukichoma tu, lazima ule chakula au sukari yako itashuka sana (hii ndio nimezungumzia hapo ju unachoma kutokana na kiwangu chako cha sukari).
Sasa kwa nyumbani kwa vile maisha ni magumu na sio wote wanaweza kumudu gharama za kuangalia sukuri kila siku, ni vizuri kwanza kufanya japo kipimo kwanza hili ukishajua ujaribu kumudu ugonjwa kwa njia ya chakula na mazoezi. Na ukiona mtu mwenye dalili za sukari kushuka sana basi mpe juisi au pipi kuokoa maisha yake kama anafahamu bado na kuweza kumeza. Usijaribu kumpa kitu chochote mdomoni kama hajitambui kwani unaweza juleta matatizo zaidi, mpeleke kwenye hospitali ya karibu mara nyingi kuna sindano wanaweza kumchoma kufanya sukari yake ipande. Kutaka kujua kama mgonjwa wako ana uwezo wa kujitambua kidogo kabla kumpa kitu mdomoni muulize maswali madogo rahisi kama jina lake, jina la rais, au leo siku gani.