Naomba kujua debe 1 ni sawa na kilo ngapi?

Salumsas

Member
Joined
Jun 19, 2020
Posts
39
Reaction score
62
Habari wakuu.

Leo naomba kujua debe 1 ni sawa na kilo ngapi?

Natanguliza shukrani!.
 
Debe 7 ya mahindi inarange 125kg mpaka 128kg ...... So Piga Mahesabu utajua Debe 1 Ina Kg Ngap
 
Dah maswali mengine kabla hujamjibu muuluza swali lazima wazo la kumtafakari muuliza swali likuijie kichwani.
 
Kg 20, kwa mazao yanayouzwa kwa kupima uzito kwa kg mfano mahindi, mchele, maharage, vitunguu swaumu, n.k mazao mengine yanapimwa kwa kuangalia ujazo (volume)...
 
Safi kabisa! Debe la mahindi maharage kunde etc ni 20kg au close to 20!

Yeye anamaanisha debe la nini[emoji3][emoji3]
 
Habari wakuu.

Leo naomba kujua debe 1 ni sawa na kilo ngapi?

Natanguliza shukrani!.
Inategemea debe la nini .
Kwa mfano debe kama lile la kunyea jela lina kilo toafauti na debe la mafuta ya kula.
 
Habari wakuu.

Leo naomba kujua debe 1 ni sawa na kilo ngapi?

Natanguliza shukrani!.
Inaonekana ulikimbia hisabati. Debe kama lilivyo, linapima volume (ujazo). Kama unakumbuka swali, debe la unyayo, na debe la mawe lipi kubwa? Hakuna kikubwa tukiongelea ujazo. Yote yana ujazo sawa wa debe 1.

Weight (uzito) ni kitu tofauti kabisa na debe halipimi huo uzito ambao ww ndio unataka kuujua kwa kilo.
Ili kujua uzito, tafuta mizani tu. Hakuna solution nyingine hapo. Nenda kwa muuza na debe, jaza debe lako, weka debe juu ya mizani, ndio ujue ni kilo ngapi.

Mizani ya kuning'iniza ni nzuri zaidi na hiyo itabidi uweke debe ndani ya mfuko wa safleti ndio ulining'inize kwa mizani na kupima.

Naongelea mizani kama zile ziko mashine wanapimia uzito wa mahindi ya kusaga nk.

Pia kumbuka madebe wengine wameyachakachua na kuyapunguza kina.
 
Haujamelekeza kuwa total weight inabidi atoe na uzito wa debe tupu jumlisha uzito wa ufuko wa sarufeti ili apate uzito halisi wa kitu alicho pima.
 
Debe haliwezi kukupa uzito(weight) wa kitu, debe linapima ujazo(volume). Debe lenye ujazo wa lita 20(20cc) linaweza kuweka mahindi yakawa na uzito tofauti na debe hilo hilo likiwekwa mtama.
 
Back
Top Bottom