View attachment 824321
Nimeambatanisha Proforma Invoice. Kwa wale wenye uelewa na mambo ya kuclear mzigo bandarini je, itanigharimu kiasi gani kuutoa mzigo bandarini?? Bado sijailipia nimewasiliana na supplier kwenye alibaba kuwa nitafute kwanza agent nijue gharama za kuutoa mzigo ndio nilipie mzigo utumwe. Asante wadau.
Gharama za ku-clear incubetor yako bandarini ni kama ifuatavyo;
1.Gharama za wakala wa meli (local shipping line agent/consolidator) haizidi $290 (Delivery Order fee, de-consolidation, sumatra charges, car service charges etc).
2.Gharama za bandari;
a). Handling charges, ambayo rate yake ni $7 plus VAT per CBM (Cubic Measurement yaani Urefu x Upana x Urefu). mfano incubetor ina
CBM 1.90, kwa hiyo handling charges: (1.90 x $7) + VAT = $15.694
b). Corridor Levy, ambayo rate yake ni $0.3 plus VAT per CBM, kwa incubetor inakua: (1.90 x $0.3) + VAT =$0.58
c). Wharfage charges, ambayo kwa sasa TRA wanaikusanya kwa niaba ya Bandari, rate ya wharfage ni 1.6% ya C.I.F value. Incubetor ina CIF value $700+10=$710, wharfage charges: ($710 X 1.6%) + VAT =$13.41.
3. Ushuru-TRA:
a) VAT -------18% ya CIF value.
b) Rail Development Levy (RDL)---1.5% ya CIF.
c). Customs Processing Fee (CPF)---0.6%.
Note, Import Duty kwa incubetor ni asilimia sufuri (0%).
4. Mwisho mkuu ni gharama za uwakala (agency fee), kampuni yangu itaku-charge tsh.150,000) na tunapatikana kwa anuani ifuatayo;
S.A Link Traders Ltd (clearing & forwarding company)
2nd Floor-Elite City building (Opposite Harbor View Tower),
Samora Avenue/Morogoro Road,
Dar es Salaam- Tanzania.
Email:
info@salink.co.tz
Mob: +255718 866 651 ( Call or Whatsapp )
Website:
www.salink.co.tz
Facebook page: S.A LINK Traders LTD