Naomba kujua gharama za ujenzi wa nyumba ya kisasa

Kama hii hapo ishakula 30M,

Ila nlichojifunza ni kuwa ujenzi wa nyumba unakatisha tamaa sana hasa kama hela yako ni ya kuunga unga.
 
Nahitaji tofali za kuchoma dar nitapata wapi?
 
Mkuu kupata hizo hesabu ni rahisi sana,ila kwa vile wewe ni kaka yangu nitakupa ushauri ufuatao,kwani kwa mpangilio wako wa bajeti kwa kutegemea taarifa finyu kama hizo,utapata ongezeko kubwa la thamani ya mradi.
1.lazima uwe na picha kamili ya unachokitaka hata kabla ya kuanza ujenzi i.e ramani yenye site plan,floor plan,views za sections,roofing,elevations,rear na front,3d views
2.ujue aina ya materials utazotumia i.e cement,mawe,aina za tofali,aina za vigae,aina za rangi,aina ya ceiling board,aina ya roofing sheet,aina za openings
3.chagua unataka mafundi wa ubora upi katika kila hatua ya ujenzi
4.muda gani utatumia kukamilisha ujenzi
 
Big up Mkuu na hongera sana, tatizo linakuja unapokuwa huna mtu wa kusimamia lazima cost zitakuwa juu sana.
 
Mkuu unambishia hadi mtu aliyetoa pesa yake mfukoni kufikia hapo..

Ndio nimemwambia inawezekana alikuwa anajenga kwa simu au alikuwa anawapa watu tu hela, boma la vyumba vitatu, master moja, public toilet, jiko na store(standard house) huwa ni 10m ukisimamia mwenyewe vizuri ila ukijenga kwa simu au kutoa tu hela itakuwa 20m. Nina uzoefu na ninachokiongea..
 
Vyumba 6 vyenye madirisha 10 ni Dar es Salaam au mkoa wenye baridi? 24M? Mkuu tupiamo kapicha tafadhali.
 
Unachosema ni sahihi. Mm nimefikia hapo kwa sh 19,450,000.
1 - ni usimamiaji wakati wa ujenzi, hapa komaa mwenyewe mara zote. Usipokuwa makini utamaliza boma la vyumba 3 naye fundi ana boma la vyuma 2,
2 - gharama za materials unaponunua navyo kama nondo, cement, kokoto, maji n.k,
3 - gharama za ufundi nazo hazipo constant na kusababisha kusiwe na uhalisia wa gharama za majenzi.
Kumbuka kwenye ujenzi wa wenye vipato vya kuunga unga mhimu kuwa na kiwanja na ramani ya nini unataka nyumba iwe, then ingia vitani. Issue ni kuwa unataka kujenga kwa mda mfupi au no limited time.
 
Inategemea n.a. design ya nyumba utatumia.material gani, na unafundi gani,

Lakin kwa nyumba uliyotaja ya siasa kuisha kabisa 30 millions
 
Mkuu unambishia hadi mtu aliyetoa pesa yake mfukoni kufikia hapo..

UNAONA HUYU MDAU CHINI, AMEKUBALIANA NA NILICHOMWAMBIA HUYO JAMAA NA KALETA USHAHIDI.

Unachosema ni sahihi. Mm nimefikia hapo kwa sh 19,450,000.
1 - ni usimamiaji wakati wa ujenzi, hapa komaa mwenyewe mara zote. Usipokuwa makini utamaliza boma la vyumba 3 naye fundi ana boma la vyuma 2,
2 - gharama za materials unaponunua navyo kama nondo, cement, kokoto, maji n.k,
3 - gharama za ufundi nazo hazipo constant na kusababisha kusiwe na uhalisia wa gharama za majenzi.
Kumbuka kwenye ujenzi wa wenye vipato vya kuunga unga mhimu kuwa na kiwanja na ramani ya nini unataka nyumba iwe, then ingia vitani. Issue ni kuwa unataka kujenga kwa mda mfupi au no limited time.

Umetumia msingi wa mawe au tofali, kama tofali idadi yake ni ngapi na kama mawe ni trip ngapi?
 
Kwa nyumba yenye ukubwa wa mita 10.85 urefu na upana 8.95 mita , ambayo imekadiliwa kuchukua tofali za block 1074 kwa msingi pekee wa kozi 6 . je nikitumia mawe naweza gharamika trip ngapi? nyumba ina vyumba 3, kimoja master, dining, kitchen,store,sitting na public toilet.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…