Naomba kujua Historia mwandishi mkongwe Ahmed Rajabu

kimbisi mbisi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2015
Posts
508
Reaction score
132
Ahmed Rajabu.
Mi naomba kuuliza kwa wenye kujua na hasa wafatiliaji wa vyombo vya habari kwa ujumla wake, kuna huyu mwandishi mkongwe aitwaye Ahmed rajabu, kwa mda mrefu nimekuwa nikiona anaalikwa na vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya uchambuzi wa mambo mbalimbali hasa yanayotokea afrika, mashariki ya kati ,ulaya na asia.kwa kweli ananivutia sana, nilikuwa naomba kujua elimu yake,historia yake, kaanzia wapi kikazi n.k na je analipwa anapoojiwa au anajitolea?,yangu ni hayo, naomba kuwasilisha,ahsanteni.
 
Mmoja wa wazanzibar wenye akili sana. Alisoma kabla ya mapinduzi ya Zanzibar. Aliondoka nchini mapema miaka ya sitini. Alienda kufanya kazi BBC na baadae kuwa mhariri wa magazet makubwa yaandikayo kuhusu afrika. Ana masters. Anajua lugha nyingi ukiondoa kiswahili. Anajua English fasaha; kifaransa fasaha;kiarabu fasaha na kireno. Hizi anaongea kama wew unavyoongea kisukuma mana kiswahili pia wengi hatujui. Yeye kiswahili anakijua kwa kukiongea na kukiandika kwa ufasaha. Ndio maana makala zake kwenye raia mwema unaweza ukadhani kakosea kumbe ndo kiswahili hasa.
 
huyu jamaa makala zake ni tamu sana.kuna kipindi nilikua simuelewi lakini baada ya kuanza kumfuatilia makala zake bila kukosa nikaanza kumuelewa.kwa kweli kwangu ni among the best writers ambao wananisisimua kwenye maandishi yao.
 
Yumo humu na Id yake ni maarufu tu ila sheria za jf zinanibana kumtaja
 
Kwangu mimi huyu ni mwandishi na mchambuzi bora wa mambo ya kisiasa na mambo mengine kwa ujumla wake katika kizazi chake. Huwezi mfananisha na wale wachambuzi uchwara kama profesa Bana wa pale UDSM

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Ahmed rajab ni msomi mzuri wa siasa za dunia hii.nafurahi sana ninaposoma makala zake na pia kumsikiliza akichambua hoja mbalimbali za kimataifa.anaifahamu sana historia ya uingereza huyu mswahili wa zanzibar.
 
Mimi anachoniudhi ni kuwa haandiki vitabu

huyu anahitaji kuandika vitabu tele kwa faida ya vizazi vijavyo
 
Mmoja wa wazanzibar wenye akili sana. Alisoma kabla ya mapinduzi ya Zanzibar. Aliondoka nchini mapema miaka ya sitini. Alienda kufanya kazi BBC na baadae kuwa mhariri wa magazet makubwa yaandikayo kuhusu afrika. Ana masters. Anajua lugha nyingi ukiondoa kiswahili. Anajua English fasaha; kifaransa fasaha;kiarabu fasaha na kireno. Hizi anaongea kama wew unavyoongea kisukuma mana kiswahili pia wengi hatujui. Yeye kiswahili anakijua kwa kukiongea na kukiandika kwa ufasaha. Ndio maana makala zake kwenye raia mwema unaweza ukadhani kakosea kumbe ndo kiswahili hasa.

Ahsante sana mkuu kwa majibu yako muruwa, pamoja na wengine walojitahidi kunijibu, shukrani, roho yangu imesuuzika, mungu awabariki.
 
Back
Top Bottom