Naomba kujua historia ya Urusi

Ziroseventytwo;eebwanae,! Umesema vema. Sasa mkuu naomba kuuliza swali linalohusu uchumi.

Mimi si mchumi ila nitakujibu kwa kadri ya uelewa wangu


1. Mbali na mafuta na gesi russia(urusi) wanategemea nini zaidi kiuchumi.

Mrusi anategemea biashara ya Silaha hasa kwa nchi za North Africa(The Maghreb)na south East Asia,pia ni muuzaji mkubwa wa diamond European Union.
Kwa bahati mbaya uchumi wa Urusi uko Vulnerable kwasababu haja diversify uchumi wake hivyo anategemea sana import ya goods kutoka European Union.


2. Yanapokutana mataîfa tajiri duniani utasikia: mataifa tajiri 8 (G8) yanayoongoza kwa viwanda pamoja na urusi/russia yatakutana labda davos. Swali. Russia siyo nchi ya viwanda.

For the record G8 is not a formal International Organisation kwasababu hakuna mkataba wowote ambao wameusaini kutengeneza G8. Hivyo usiringanishe G8 na NATO au European Union.
And Yes my friend Russia is an industrialized country. The main difference is that Russia haven't invested much in Super-Civilian Technology.

3.pesa ya russia inathamani gani ukiilinganisha na dola ya u.s.a au na hata euro ya nchi za ulaya?

Without being prejudiced Russian Ruble haiwezi kushindana na Dollar, Euro and The Pound. At least Not for Now.
Hii ni kwasababu Dollar ndiyo the main Currency inayotumika sana ila kufacilitate international trade and exchange.
The Dollar Diplomacy Started during the 1947 all the way to the 1990's during the collapse of the soviet union.
Kumbuka matajiri wengi wa Urusi hata pesa zao wamewekeza nje katika nchi za ulaya hivyo ni ngumu kuifanya currency yao Ruble ishindane na Dollar.

But in the near future inaweza kushindana kwasababu kuu mbili

  1. The Existance of The BRICS
  2. The Formation of The Asian Development Bank under China.
Mwaka huu huu China-Urusi wamesaini deal la Billions and unfortunately wametumia Rubles and Chinese Yuan.
Vivyo hivyo kwa matifa mengine.

Na la pili Bank hiyo hata muingereza na mataifa mengine wanazungumza kujiunga ambapo kupata mkopo ni lazima utapewa kwa currency za Asia hivyo ni lazima Yuan Diplomacy ita weaken the influence of the dollar in Europe.



CC: Abu mohamed , Mchumba, Globu , Ziroseventytwo , mtoto wa bata , ROBERT MICHAEL , saidi yande , Mahesabu , Bayyo , Tanzanite klm , Vlad , t blj , Walas Ba , majeshi 1981 , JustDoItNow , toto zuli , born again pagan , kireri jr , shabani hassani , Ngongo , Mashy Jim007 2 , utafiti , Dotworld , maziku masunga Jr, Bukyanagandi
 
Walas Ba;Shukran mkuu emporar

Maswali

1.Alievujsha siri za urusi kwa western alaifanya ivo ili kuisliti nchi yke au alipandikizwa?

Huyu aliisaliti nchi yake.
Huwa wanitwa defectors. Alidai kwamba hakuridhika na utawala wa Kikomunisti kipindi kile.

2.Kwan mambo muhimu karibu yote ya Urusi yana herufi ''v" kuna utukugu gani kwenye herufi hii au kuna maana gani hasa kwao.

Hili halina Ukweli wowote. Kwasababu lugha za watu wa Slavic region au Eastern Europe zina baadhi ya alphabets zilizoongezwa.
Kama kipolishi kina alphabets za lugha ya kilatini zilizoongezwa.


3.Jehistoria inasema nn kuhusu kuweza kutokea kwa vita nyingine ya dunia?

Siwezi kusema ndiyo au hapana.
Kwasababu History is a place of reference and not a place of residence
Ila mengi hutokea.

4.Uchumi wa urusi unauwezo wa kumudu vikwazo vya marekan?

Indeed. Kwasababu zifuatazo,

  1. kwasababu Urusi ndiyo soko kubwa la European Union
  2. Marekani anategemea sana ushawishi wa kidipomasia wa Urusi hasa katika nchi za mashariki ya mbali kama Iran and Syria
  3. Urusi ana mbadala ambao ni THE BRICS
  4. Mwisho, Vikwazo vikizidi vitaleta mtafaruku duniani na hata Mataifa ya Ulaya yanajua hilo.
Amani ya duniani inategemea ushawishi wa mataifa makubwa kama China na Urusi.
 

Mkuu nimekukubali
 
Last edited by a moderator:
Bandiko zuri lakini kuna sehem umepotoka..si kweli kwamba Taifa la israel lilitakiwa liundwe east africa...la sivyo km una nondo weka tupite nazo
 
Bandiko zuri lakini kuna sehem umepotoka..si kweli kwamba Taifa la israel lilitakiwa liundwe east africa...la sivyo km una nondo weka tupite nazo

Haya kwa kukusaidia tu hebu soma hiyo nyaraka, uone jinsi Gavana wa makoloni wa Uingereza Lord Chamberlain alivyofanya kikao pamoja na viongozi wa Zionist Congress mwaka 1903.
Akipendekeza wayahudi wanaoishi Urusi wapelekwe Uganda at that time inaitwa British Uganda.
Ilishidikana na haikuwezekana.

Miaka ya 1930's serikali ya Ujerumani chini ya Hitler ilitaka Jewish State iwe Madagascar ila ikashindikana pia kwasababu Muingereza ailikuwa na ajenda zake nyingine.




Sources: Encyclopedia of Genocide and Crimes Against Humanity, Encyclopedia of the Age of Emperialism Vol1&2,
Cambridge History of Modern World Vol 1, Cambridge History of the Cold war vol 1&2.
Links:http://www.jewishvirtuallibrary.org/jsource/Zionism/Uganda.html

Nadhani nimekusaidia mkuu

cc: mtoto wa bata , Dotworld , Globu , Mahesabu , born again pagan
 
Last edited by a moderator:
historia ya kupendeza sana kaka..mojawapo ya sifa kubwa sana za warusi ni kutengeneza vitu simpo, rilayabo na vinavyofanya kazi iliyokusudiwa (kwa wale waliopitia jeshini wanaelewa hii makitu sana-bunduki mizinga vifaru na nyambizi NATO walizibatiza "blackholes" manake walikuwa wanshindwa kuzi ditekti mahala zilipo kwenye bahari za pacific na atlantic, midege yao ya MiG ilikuwa inatumia Vacuum tubed radar systems ingawa marubani wa NATO walikuwa wanawabeza hapo mwanzoni lakini walikuja gundua kuwa radar za aina hii z inaathiriw kidogo sana na electronic jamming system, ingawa na zenyewe zilikuwa na ishu zake baadae warusi waliziacha pia---wataalam zaidi wataongezea ama kusahihisha)
 

Very simple,
Hasa kwenye Vacuum tubed radar systems.
Hapa ndiyo utakuja kujua umuhimu wa kuwekeza kwenye elimu.
 

Kuna kitabu, Khrushchev Remembers,'' kaandika mwenyewe ni kitabu kizuri kwa kuielewa siasa za Urusi kabla na baada ya mapinduzi. Pia kuna movie, ''Nicholas and Alexandria,'' kuna mengi ya kujifunza.
 
Last edited by a moderator:
Kuna kitabu, Khrushchev Remembers,'' kaandika mwenyewe ni kitabu kizuri kwa kuielewa siasa za Urusi kabla na baada ya mapinduzi. Pia kuna movie, ''Nicholas and Alexandria,'' kuna mengi ya kujifunza.

Shukrani sana Mkuu.
 
COLD WAR: PHASE 1- The Bolshevik Revolution and Versailles Treaty

Okay Champs,
Tuanze kuzungumzia vita baridi A.K.A The Cold War.
Kama alivyosema @born again pagan pagan.
Ntajaribu kulelzea kwa kadiri ya uwezo wangu.

Kwanza neno lenyewe Cold War lilitengenezwa na mwandishi mashuhuri mwenye asili ya Uingereza anaitwa George Orwell. Hii ilitokea baada ya Marekani kuangusha mabomu ya atomiki huko japan katika matimbo ya Hiroshima na Nagasaki. Hii ilikuwa ni kumaanisha vita isiyohusisha majeshi ya nchi kubwa kwa moja kwa moja ila tu wanatumia nyanja nyingine kama uchumi na kisiasa (ukomunisti na Ubepari), propaganda na ukusanyaji wa taarifa za kiintelijensia ili kumtishia adui yako.

Hasa kwa ufupi tu, wataalamu wanaanza kusema Cold-War ilianza mara baada ya mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1917. Haya mapinduzi kama nilivyoelezea hapo awali katika toleo la kwanza yalileta sera mpya kabisa duniani inayoitwa ukomunisti. Ukomunisti kwa kifupi ni ujamaa uliokamaa; Hii ni sera ya kiuchumi na kisiasa inayofanya mifumo yote ya kimaisha ya nchi kuwa chini ya utawala la kiraia ili kujenga usawa na kuondoa aina yote ya matabaka.

Hii sera ilionekana ni hatari sana kwa mataifa ya Magharibi kwasababu moja kubwa; Hii sera ili iweze kufanikiwa kama aliyeitunga Karl Marx ni lazima dunia yote iwe chini ya ukomunist. Hivyo basi kulikuwa na mpango wa Warusi kupeleka mapinduzi katika nchi za Ulaya, Marekani, Asia na Mwishowe Afrika.
Hili likawa tishio sana kwa mfumo wa kimaisha wa Ubepari hivyo baada ya mapinduzi ya Urusi na vita ya kwanza ya dunia kuisha kulikuwa na Civil War kubwa sana ndani ya Urusi ambapo ule utawala wa watu wachache wanaoijiiita THE WHITES ilipigana na utawala mpya wa Kibolshevik waliojiita THE REDS.
Hawa THE WHITES walisaidiwa na mataifa ya Magharibi kama Marekani chini ya raisi Woodrow Wilson, Ufaransa chini ya George Clemenceau na Uingereza chini ya Waziri mkuu aliyeitwa Lloyd George.
The Bolsheviks wao walisaidiwa sana na Ujerumani amabao walikuwa maadui wa nchi nyingi za Magharibi.

Mwishowe hiyo vita iliishia vibaya baada ya The Whites kushindwa na Mataifa ya Magharibi yakashindwa kuua ukomunisti katika hatua ya kwanza katika miaka ya 1918-1919.
Baada ya hapo ulifanyika Mkutano wa Versailles Ufaransa 1919 ambapo mataifa ya Ulaya yalitoa adhabu kali kwa Mjerumani kwa kusababisha vita ya Kwanza ya dunia.
Katika makubaliano hayo Mjerumani aliumizwa sana kiuchumi na mataifa ya Marekani, Ufaransa na Uingereza kufaidika sana.
Katika mkutano huo walitengeneza Umoja wa mataifa unaitwa The League of Nations ambao uliyatenga mataifa makubwa kama USSR na China.


Ikumbukwe kipindi hichi the world super power alikuwa na Muingereza bado ambapo kitakwimu alikuwa anamiliki asilimia zaidi ya 21% ya Ardhi ya Dunia. Hii ni katika makoloni yake yote ya Asia, Amerika na Mashariki ya kati. Huu ulikuwa ni utajiri mkubwa sana na ulimfanya muingereza ainyonye dunia ipasavyo.
Kipindi hichi Urusi na Marekani walikuwa na influence ndogo ukilinganisha na ya muingereza, ufaransa, Uturuki kipindi hicho ni Ottoman Empire, Japan, Belgium na Spain. Hivyo ikawa ngumu sana kwa mrusi kujitanua ipasavyo.

Huu ndiyo mwisho wa Utangulizi wa Cold War.
Stay tunned for the Second Phase.

BY: MALCOM LUMUMBA a.k.a COBBLEPOTS
 
Last edited by a moderator:
COLD WAR: PHASE 2- Stalin's Russia.

Vladmir Illyich Lenin kiongozi wa kwanza wa USSR alikufa mwaka 1924. Ikumbukwe aliukuwa anaumwa kisukari na alishanusurika na vifo vya risasi mara mbili tofauti hivyo kupelekea afya yake kuzorota hadi kufa.
Lenin alipenda arithiwe na Leon Trotsky ambaye alikuwa ni rafiki yake wa karibu na ndiye aliyetengeneza muundo wa jeshi la Urusi The Red Army pamoja mifumo ya kiintelijensia kipindi hicho ambayo ilikuwa ni The Cheka baadae uliitwa OGPU,NKVD,NKGB,KGB ambao saa hizi inaitwa FSB na SVR. Pia alisaidia sana kutengenezwa kwa chombo cha kijeshi cha upelelezi (Military Intelligence) ambacho mpaka leo hii kipo kinaitwa The GRU.

Leon Trotsky alikuwa ni Myahudi na kipindi hicho wayahudi wengi walikuwa wanatengwa sana Urusi. Hivyo Stalin pamoja na genge lake waliwawahi wakina Trotsky na kundi lake hivyo Joseph Dhughashvili A.K.A Comrade Joseph Stalin akawa kiongozi wa Urusi.
Stalin alitofautiana na Lenin na Trotsky katika kusema Ukomunisti ni lazima uimarike kwanza USSR kisha Upelekwe katika mataifa mengine.
Katika hili Stalin alikuwa sahihi kwasababu bila kufanya hivyo Urusi isingeweza kushinda vita ya pili ya Dunia na umoja ungekuwa umesambaratika mapema.

Stalin alianza FIVE YEARS PROGRAM ambapo alianza kuimarisha Uchumi wa Urusi kwa ajili ya kutawala dunia. Aliongeza kasi ya watu kupata elimu hasa aliwekeza sana katika Upelelezi wa Kiviwanda unaoitwa CORPORATE ESPIONAGE na Military Intelligence. Katika haya majaribio ya kipelelezi Moscow iliweza kupandikiza Majasusi wengi Ulaya, Asia na Marekani.
Ikumbukwe baada ya mapinduzi ya Urusi kulikuwa na wimbi kubwa la wakimbizi kutoka Urusi kuelekea mataifa mbalimbali ya Ulaya. Hivyo walipokelewa vizuri na kupewa Uraia wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Hispania, Ujerumani, China na mataifa mengi.

Moscow ilitimia mwanya huu kupenyeza majasusi katika nchi za Magharibi hasa katika Viwanda, majeshi na serikali. Hawa wanaitwa SLEEPER AGENTS ambao wao kazi yao ilikuja kuonekana wakati wa vita ya pili ya dunia na baada yake.
Mataifa ya Magharibi yaliupuuzia umoja wa nchi za Kisovieti kwasababu ulikuwa ni maskini sana kiuchumi na mbaya zaidi mwaka 1919 Urusi walishindwa vita na Nchi ya Finland hivyo ikawa ni aibu.

Huku nyumbani Stalin alitengeneza kitu kinachoitwa A Closed Society, ambapo mfumo wa kijasusi wa Urusi ulikuwa katika kila kona na kila kitongoji. Kuanzia walimu, wanafunzi, wanajeshi, airport, walinzi wa mipaka,raia wa kawaida na nk.
Stalin alisaini mkataba unaoitwa THE CONCORDE AGREEMENT ambao uliwazuia vijana wa Urusi chini ya miaka ya 40 wasitoke nje ya URUSI; hii ilisaidia sana kuzuia influence ya magharibi nchini Urusi lakini pia ilikuwa inapunguza maendeleo ya kasi nchini humo kwasababu haukuwa unasaidia innovation na biashara.

End of Phase two; stay tuned for phase 3

BY: MALCOM LUMUMBA a.k.a COBBLEPOTS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…