Jaslaws, mm ktk mada yako nina haya yakuchangia ktk kujibu maswali yako;-
je wabunge wakipiga kula ya vote of no confindence kwa raisi bunge linavunjwa? - Hapana bunge halitovunjwa, sababu ili bunge livunjwe Katiba imetoa ni wakati gani Rais anaweza kulivunja Bunge kwa mujibu wa sheria ambayo ipo kwenye Ibara ya 90 (2). Hivyo basi mbali na hiyo Rais hawezi kulivunja Bunge kwa mujibu wa sheria, hata kama wabunge wamepiga kura ya kutokua na imani naye. Manake hapo Wabunge watakua wametumia haki yao ya Kikatiba kwa mujibu wa Ibara 46A ambayo imetoa mchakato mzima mpaka Rais anapotoka madarakani kwa kushitakiwa. Kwa faida yetu wote hapa Katiba inasema "......Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshitaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii"
mbunge atapoteza sifa ya kua mbunge pale raisi atakapolivunja bunge kama ilivoonyeshwe katka ibara ya 90(2)(a mpka e)? - Hapana hawezi kupoteza sifa za kuwa Mbunge, sababu sifa za mtu kuwa Mbunge zimeelezwa kwenye Ibara ya 67 (1) na kwa Rais kulivunja Bunge hiyo haimuondolei mtu au mbunge sifa za kuwa mbunge. Sababu ambazo zinamfanya mtu kukosa sifa za kuwa Mbunge zimeainishwa kwenye Ibara ya 67 (2).
Hivyo ndio navyoona kwa mujibu wa maswali yako.