Naomba kujua jinsi ya kuongeza salio UTTAMIS

Magni

New Member
Joined
Jul 11, 2021
Posts
2
Reaction score
0
Habari za wakati huu
Naomba msaada juu ya mfuko wa uwekezaji ukwasi , jinsi ya kuongeza salio katika account yako ya uwekaezaji kupitia simu, na ni faida gan ninazozipata ninaponunua vipande au kuuza vipande.
Ahsante
 
Website Yao ina maelekezo yote hususani estimated returns plus njia zote za ku deposit za simu na bank.

Sent from my 21051182G using JamiiForums mobile app
 
Hao jamaa nilifungua account nikaweka na hela nilishindwa ku log in na niliweka elfu 7000.nimefika crdb napo nilienda kujaza form lakini mpaka leo hamna updates. Customer care hamna kabisa maana hata simu hawapokei.
 
Habari za wakati huu
Naomba msaada juu ya mfuko wa uwekezaji ukwasi , jinsi ya kuongeza salio katika account yako ya uwekaezaji kupitia simu, na ni faida gan ninazozipata ninaponunua vipande au kuuza vipande.
Ahsante
website yao inavikokotoo unaweza kuangalia ukajua ukiweka kiwango flan kwa mda flan unaweza ukapata kias gani..
 
nimewekeza mifuko minne ( bond, jikimu, umoja na ukwasi).. mdogo mdogo tu.. ila uwekezaji wa huku unahitaj uvumilivu wa hali ya juu... maaana ni mambo ya compound interest
 
Haina haja kuwa na mifuko mingi, weka mfuko mmoja au miwili yenye tija upate interest nzuri
 
Hao jamaa nilifungua account nikaweka na hela nilishindwa ku log in na niliweka elfu 7000.nimefika crdb napo nilienda kujaza form lakini mpaka leo hamna updates. Customer care hamna kabisa maana hata simu hawapokei.
*150*82#
Ingiza namba yako ya siri ya simInvest ambayo ulisajiri nayo
Utafika kwenye dondoo zinazokupa maelekezo (hapa chagua #7)
Utaulizwa mtandao ziliko pesa zako kama Tigo, Mpesa au Airtel
Utaulizwa namba ya akaunti unakotaka kuweka
Kisha weka kiasi cha pesa
then you go!
 
Haina haja kuwa na mifuko mingi, weka mfuko mmoja au miwili yenye tija upate interest nzuri
nlitaka kukuza mtaji sio wa wekeza maisha so kuna mifuko inachangia wekeza maisha sio lazima niwe naweka kila mwez
 
*150*82#
Ingiza namba yako ya siri ya simInvest ambayo ulisajiri nayo
Utafika kwenye dondoo zinazokupa maelekezo (hapa chagua #7)
Utaulizwa mtandao ziliko pesa zako kama Tigo, Mpesa au Airtel
Utaulizwa namba ya akaunti unakotaka kuweka
Kisha weka kiasi cha pesa
then you go!
Aisee niliingiza mara nyingi nikafungiwa
 
nimewekeza mifuko minne ( bond, jikimu, umoja na ukwasi).. mdogo mdogo tu.. ila uwekezaji wa huku unahitaj uvumilivu wa hali ya juu... maaana ni mambo ya compound interest
Kwa mfuko wa Jikimu, gawio ni Tsh ngapi kwa alieweka 2M (gawio ni kila robo mwaka)
 
kwa miaka minne ya nyuma haiajwahi kushuka 10% na kuna mwaka ilienda hadi 12%.. so pigia kwa mwaka 10% ili kutokuwa optimistic saaana.. igawe mara nne.... kwa hiyo ni kama 2.5% ambayo kwa uwekezaji wa 2M ni kama 50K
 
Back
Top Bottom