Naomba kujua jinsi ya kupika michembe

Naomba kujua jinsi ya kupika michembe

Michembe ndio mi nin?
Viazi vitamu vilivyokaushwa juani.

Michembe.jpg
 
Msimu wa mchembe umeanza nini. Hii kitu ninoma sana pale inapokutana na chai ya maziwa.
 
Zioshe, weka kwenye sufuria then weka maji mengi ili ziive vizuri, zikiiva soga kama ugali, then tayari kwa kula
Aisee nashukuru sana. Nitaufanyia mambo na kuleta ushahidi wa Picha mnato. Tunakula na nini hapo cha kusukumia
 
Kumbe huwa yanapikwa hayo makitu nilijua yanaliwa hivyohivyo.
 
Huu utaalamu tumuombe ngosha the don SHIMBA YA BUYENZE

Japo sijaelewa mleta mada kaomba nini maana kuna kuitengeneza michembe toka kwenye viazi au ana michembe tayari anataka kuipika
Hahaa. Yabidi huyo Ngosha atuelekeze kwa kweli.

Nilivyoelewa ni kwamba ana michembe ila anataka afundishwe namna ya kuipika.
 
Hahaa. Yabidi huyo Ngosha atuelekeze kwa kweli.

Nilivyoelewa ni kwamba ana michembe ila anataka afundishwe namna ya kuipika.
Ni kweli Mkuu.
Jana usiku nilikamilisha zoezi LA kupika hiyo bidhaa na asubuhi na mapema nimeitwanga nikisindikizia na herbal tea na machungwa.

Niliiloweka kidogo. Nikaichemsha muda kadhaa hapo nilipitiwa ikaungua. Nikafuata maelekezo ya mkufunzi hapo juu kuisonga kam ugali.

Ilikuwa vzr sana ila shida sijajua kama inawekewa Chumvi au sukari imebidi niiache hivyohivyo nyutro. Leo jioni nitaimalizia Maana sijawahi kula hii kitu before.
 
Kikwetu kwetu

Matobolwa - ni chakula kitokanacho na zao la viazi, viazi vikivinwa vinaanchwa visinyae kupunguza maji na baadaye vinapikwa na kuipuliwa Kisha kukatwa katwa na kuanikwa vikikauka binahifadhiwa tayari kwa matumizi.

Mchembe - ni zao la viazi hivi utofauti na matobolwa vyenyewe havipikwi tu vinamenywa na kikatwakatwa na kuanikwa tayari kwa chakula

Matumizi

Ni chakula kizuri kitamu sana
Mchembe unaweza saga na kupika Kama uji, au ugali au vilevile

Kwa kutumia na karanga zilizokaangwa, au mbegu za maboga au bhupandya hahahah + mtindi hitasahau
 
Jinsi ya kupika Michembe.
1-Chukua Michembe inayo tosha kwa ajiri ya kupika, osha(Unaweza osha na maji ya vuguvugu/ya baridi).
Harafu ziache.
2-chemsha maji haya Ni kwaaji ya kupikia. Kisha weka kwenye chombo.
3-weka maji kwa kukadilia yatakayo tosha kupikia Kisha weka Michembe kwenye hayo maji na weka chumvi kidogo bandika.
4-funika kama unapika mboga utakua unaangalia maji yakioelea ongeza, hadi zitakapo iva.
5-Zikisha iva anza kupondaponda hadi ziwe laini Kisha opoa.

Hapo pishi lako la Michembe litakua Tayari.

Imeandikwa na Emmanuel Kasomi

Wakuu nimeipa hii bidhaa mahala ila sijui jinsi ya kuandaa.

Naombeni ufahamu.

Natanguliza shukrani
 
Ni kweli Mkuu.
Jana usiku nilikamilisha zoezi LA kupika hiyo bidhaa na asubuhi na mapema nimeitwanga nikisindikizia na herbal tea na machungwa.

Niliiloweka kidogo. Nikaichemsha muda kadhaa hapo nilipitiwa ikaungua. Nikafuata maelekezo ya mkufunzi hapo juu kuisonga kam ugali.

Ilikuwa vzr sana ila shida sijajua kama inawekewa Chumvi au sukari imebidi niiache hivyohivyo nyutro. Leo jioni nitaimalizia Maana sijawahi kula hii kitu before.
Next time tafuta peanut butter ile lainii ya kumiminika, Kisha badala ya kuvisonga chemsha tuu then wakati wa kula unakua unadip kwenye hiyo siagi.....ni tamu sana na addictive kiaina vile inamelt mdomoni...niliwahi kuandaliwa na rafiki yangu Mganda mwanzoni nilisita ila baada ya kuonja nilipenda kwa kweli..
 
Back
Top Bottom