Naomba kujua juu ya biashara ya M-Pesa

Naomba kujua juu ya biashara ya M-Pesa

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Watanzania, baada ya kuhangaika kutafuta ajira na kushindwa, nimeamua kuanzisha biashara ya M-Pesa.Tafadhali mwenye uzoefu na hii biashara naomba anifahamishe yafuatayo:

1.Mtaji wa kuanzia
2. Pamoja na M-Pesa naweza kuchanganya na biashara gani kwenye hicho chumba
3.Changamoto za M-Pesa
4.Faida yake.

Ni imani yangu mtanisaidia mawazo yenu.
 
CHANGAMOTO NI CHOO TU UKIPATA CHOO KARIBU NA M-PESA YAKO EVERYTHING KINAKUWA ALRIGHT
Mkuu pamoja na kuomba ushauri naomba uwe na busara hakuna atakaye kusifu kwa umama wako.
 
Mkuu pamoja na kuomba ushauri naomba uwe na busara hakuna atakaye kusifu kwa umama wako.
unaona sasa ulivyo wa ajabu!!!

huamini kama choo ni muhimu kwa hiyo biashara!haaya basi

uwe na mtaji milioni 8,bila kusahau simu ndogo 5.
 
Nahisi Kuna Uzi humu unazungumzia hii biashara

Cha kwanza unatakiwa uwe na eneo la kufanyia kazi ya m pesa

Pili uwe na mtaji kulingana na mahitaji ya Wateja wako

Tatu uwe na uelewa wa Huduma za za kimtandao

Mfano kuna promotion ya Voda na mteja antegemea wewe ndio umwelekeze zaid

NNE unaweza kufanya na biashara nyingne kulingana na mahali ulipo

Kwa mfano mahitaji ya nyumbani

Au kuingiza nyimbo kwenye memory. Frash
na kukodisha CD pia

Tano hakikisha uwe mwaminifu kwa Wateja na rugha sahihi kwa Wateja

Maana unahudumia watu wenye stress na walio na furaha ujio wao haufanani


Sita ogopa mazoea na watu usio waelewa kwenye biashara yako

Saba hakikisha unahudumia mteja kwa usahihi na umakini usimpunje asikupunje

Changamoto zipo ila hazikushindi ukiamua
 
mpimamstaafu
Anza na mtaji 1 million inatosha, taratibu utakua unapanda, usitegemee hio tu, changanya na huduma zingine kama kuchaji simu, kuuza cover za simu, eaephones, screen protectors, pia ongeza na mitandao mingine kama tigo pesa, halopesa, airtel money, pia unaweza kuchangaya hapo ukaweka kama mtaji unaruhusu, uuze na simu(teknolojia inakua sana),.pia waweza kuweka na maji either uuze jumla au rejareja, soft drinks kama soda n.k,

Kumbuka : KAULI NZURI KWA WATEJA, awe mkorofi, mpole, mzuri wa sura au umbo, wewe lengo lako ni moja kauli nzuri na uaminifu, vishawishi vipo vya wadada ila ni kua makini na malengo yako.
 
Changamoto kubwa kwenye hii biashara Ni chuma ulete , hii kitu Nina experience nayo na sijawah kupata suluhisho nikaamua kufunga biashara
Chuma ulete ni imani yako
 
Back
Top Bottom