Gearbox inatumia mafuta tofauti yanayoitwa Automatic Transmission Fluid (ATF). Sasa kuwa makini sana na mafuta utakayoweka kwenye Transmission yako. Soma kitabu cha gari yako kwa makini ujue aina ya mafuta yatakiwayo. Kuna aina nyingi sana za ATF kwa mfano Dexron (aina kadhaa), Mercon (aina kadhaa), ATF+ (ain kadhaa), Toyota ATF (aina kadhaa), Honda ATF (aina kadhaa). Ingawa kuna aina fulani fulani zinaingiliana, lazima utumie mafuta sahihi, na usizidishe au kupunguza kipimo. Ukukosea aina ya mafuta au ukakosea kipimo - yaani ukaweza zaidi ya kiasi kinachotakiwa, basi transmission yako itakufakifo cha mende!
Kuservice transmission yako, iache ipoe halafu umwage transmission ya zamani yote (ukiacha ile iliyoko kwenye Torque converter tu), halafu unabadilisha transmission oil filter, na baade kujaza tena oil mpya, usifanye tu kuongezea kwenye oil ya zamani.
Engine oil kutoka kampuni yoyote itafanya kazi tu mradi iwe aina ya 5W-30. Iwapo utahitaji kuhakikisha unaweka kila kitu sawa; weka oil aina ya 80W-90 kwenye diff pia.