Naomba kujua kamuni nzuri kwa Oil ya gear na engine

mwambyetete

Senior Member
Joined
May 17, 2018
Posts
132
Reaction score
202
Habari wakubwa,,mm n mmiliki mgen wa gar naomba kujua ni kampuni ipi nzur kwa gear na engine ambapo gari ni automatic

Aina ya gar ni toyota premio, wapo walioniambia inahitajika type iv,naipata wap na mimi niko mbeya
Pia kati ya oili za Total na castrol zipi nzur na inafaa nitumie kwa km ngap?

Tafadhali lengo sio kutangaza kwamba nnamiliki gar bali ni kupata elimu tu ,natanguliza shukran sio mbaya ukiniambia na bei zake na maduka.
 
Gearbox inatumia mafuta tofauti yanayoitwa Automatic Transmission Fluid (ATF). Sasa kuwa makini sana na mafuta utakayoweka kwenye Transmission yako. Soma kitabu cha gari yako kwa makini ujue aina ya mafuta yatakiwayo. Kuna aina nyingi sana za ATF kwa mfano Dexron (aina kadhaa), Mercon (aina kadhaa), ATF+ (ain kadhaa), Toyota ATF (aina kadhaa), Honda ATF (aina kadhaa). Ingawa kuna aina fulani fulani zinaingiliana, lazima utumie mafuta sahihi, na usizidishe au kupunguza kipimo. Ukukosea aina ya mafuta au ukakosea kipimo - yaani ukaweza zaidi ya kiasi kinachotakiwa, basi transmission yako itakufakifo cha mende!

Kuservice transmission yako, iache ipoe halafu umwage transmission fluid ya zamani yote (ukiacha ile iliyoko kwenye Torque converter tu), halafu unabadilisha transmission oil filter, na baade kujaza tena oil mpya, usifanye tu kuongezea kwenye oil ya zamani.

Engine oil kutoka kampuni yoyote itafanya kazi tu mradi iwe aina ya 5W-30. Iwapo utahitaji kuhakikisha unaweka kila kitu sawa; weka oil aina ya 80W-90 kwenye diff pia.
 
Asante saaana kaka,,,je ipi nzur kati castrol na Total?? Pia kwenye gearbox pia kuna oilfilter??
Gearbox inatumia mafuta tofauti yanayoitwa Automatic Transmission Fluid (ATF). Sasa kuwa makini sana na mafuta utakayoweka kwenye Transmission yako. Soma kitabu cha gari yako kwa makini ujue aina ya mafuta yatakiwayo. Kuna aina nyingi sana za ATF kwa mfano Dexron (aina kadhaa), Mercon (aina kadhaa), ATF+ (ain kadhaa), Toyota ATF (aina kadhaa), Honda ATF (aina kadhaa). Ingawa kuna aina fulani fulani zinaingiliana, lazima utumie mafuta sahihi, na usizidishe au kupunguza kipimo. Ukukosea aina ya mafuta au ukakosea kipimo - yaani ukaweza zaidi ya kiasi kinachotakiwa, basi transmission yako itakufakifo cha mende!

Kuservice transmission yako, iache ipoe halafu umwage transmission ya zamani yote (ukiacha ile iliyoko kwenye Torque converter tu), halafu unabadilisha transmission oil filter, na baade kujaza tena oil mpya, usifanye tu kuongezea kwenye oil ya zamani.

Engine oil kutoka kampuni yoyote itafanya kazi tu mradi iwe aina ya 5W-30. Iwapo utahitaji kuhakikisha unaweka kila kitu sawa; weka oil aina ya 80W-90 kwenye diff pia.
 
Asante saaana kaka,,,je ipi nzur kati castrol na Total?? Pia kwenye gearbox pia kuna oilfilter??
ndiyo Gearbox ina oil filter. Castrol na Total zote ni sawa tu; kinachojali ni namba zake tu
 
Back
Top Bottom