Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 576
- 876
WanaJF naomba Ushauri,Nina matatizo yanamkabili Baba yangu baada ya kufiwa na Mama yake wiki mbili zilizopita yananichanganya sana,Awali siku mbili baada ya Msiba alipata tatizo la Mkanda wa jeshi uliompiga upande mmoja wa Uso wakati huohuo akapata tatizo la Presha,awali hakuwa nayo labda kama alikuwa nayo hatukuwahi kumpima ila tulinotice baada ya kuona mdomo wake umepinda kwenda kupima Presha ikawa iko juu sana akalazwa ICU pale Regency ilikuwa 230/130,ila tatizo linalotukabili huu Mkanda wa Jeshi umeathiri jicho na haliponi ni almost Mwezi sasa,niliamua kumpima HIV,Moyo,Full Blood Count kote yuko safi,ila Sukari ambayo tunamfuatilia mara zote tumempima baada ya kunywa chai jana ilikuwa 8.7 leo tumekuta 10 sasa sijajua hii ni Sukari ya kawaida kweli?Naomba msaada kwa mnaojua.
Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums