Naomba kujua kuhusu GPS katika gari aina ya Mitsubishi Outlander

Naomba kujua kuhusu GPS katika gari aina ya Mitsubishi Outlander

BALOTEL

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
627
Reaction score
761
Habarini wadau, natumai Ijumaa yetu inakuja vizuri.

Natumia gari aina ya Mitsubishi Outlander, week iliyopita nilijaribu kuifunga GPS kwa ajili ya kuikodisha ila tangu ifungwe GPS imeanza kuonyesha tofauti fulani fulani kwenye dashboard yake.

Inabadilika kutoka 2 wheels kwenda 4 wheels wakati ikiwa kwenye mwendo na baadae inarudi automaticaly.

Sasa kwa wajuzi wa mambo haya naomba msaada wa nini cha kufanya kabla sijaanza kuwapelekea mafundi wetu hawa.

NB: Tatizo limeanza tu baada ya kufunga GPS.
 
Juzi kati hapa, Kuna jamaa yangu wa Upon tyne newcastle haliirudisha Kwa recomended Garage , kulisemekana kuna shida katika mifumo ya brake.
sijajua Tanzania tunaenda kwa nani. ila hii Gari haiitaji GPS au tracking yoyote , automatically yenyewe inajitrack.
 
Habarini wadau, natumai Ijumaa yetu inakuja vizuri.

Natumia gari aina ya Mitsubishi Outlander, week iliyopita nilijaribu kuifunga GPS kwa ajili ya kuikodisha ila tangu ifungwe GPS imeanza kuonyesha tofauti fulani fulani kwenye dashboard yake.

Inabadilika kutoka 2 wheels kwenda 4 wheels wakati ikiwa kwenye mwendo na baadae inarudi automaticaly.

Sasa kwa wajuzi wa mambo haya naomba msaada wa nini cha kufanya kabla sijaanza kuwapelekea mafundi wetu hawa.

NB: Tatizo limeanza tu baada ya kufunga GPS.
Pole sana mkuu sasa hapa huoni kwamba kikulacho kinguoni mwako??. In short ufungaji wa hiyo GPS ndio mchawi au chanzo cha kuitia ugonjwa gari yako.kumbuka hiyo gps sio original ya kutoka na gari bali ya kufunga na wafungaji wengi wao wanachojua ni kitu anachokifunga kinahitaji nn na nn kama ni power moto direct na switch on atatafuta inapopatikana na kuunga ilimladi anachokifunga kimefanya kazi bila kutambua au kujua hapo alipochukulia huo moto au kuunga waya wake pana kazi gani shida nyingi ndio huanzia hapo.. au unakuta sawa kachukua power kwenye waya flani lkn kwa kuwa hiyo gps aliyofunga ni circuit nyingine ambayo inajitegemea unakuta wakati inafanya kazi huwa kuna kuwa na current flani au signal inaludisha na kuanza kuleta shida kama hizo..

Pakuanzia tafuta fundi umeme aitoe hiyo gps then kama aliyefunga kuna waya alikata aziludishie kama zilivyokuwa then test gari uone kama itakuwa bado na shida au laa??.

Kama itakuwa shida imeondoka basi gps ifungwe vizuri.

Shida kama itakuwa bado ipo basi gari ifuatiliwe kwa umakini ikiwa pamoja na kuipima pia aina hiyo ya gari yako ni ecpensive sana na inahitaji fundi wa uhakika coz mm nishakutana nazo ukifanya mistake kidogo ikaungùza au leta shida ya stepper motor ya kwenye gearbox ndio inakuwa msiba zaidi.
0627136700 kama utahitaji msaada zaidi au ushauri na karibu pia JO AUTO TECH
 
Back
Top Bottom