Hyo ya juu ndo nzuri zaidi na ni ya kuiamini sana, ina ubora kama wa Land-cruiser mkonge kuanzia engine na uvumilivu wa barabara na speed pia, zinatulia barabarani ila hazitaki service za bei rahisi, utaponunua spare yake original jua umefunga mkataba haziharibiki kirahisi labda kama wewe ni mlevi na unavamiaga mitaro[emoji23][emoji23]
Ila model hyo kuna zenye ulaji mzuri wa mafuta mfano za 2.0 ltr cylinder 4 pia kuna za 2.4 ltr 4 cylinder ila kumbuka kuna za hvo hvo zenye engine ya V6 inakula sana mafuta ila performance yake iko vizuri sana....nakushauri uchukue hyo yenye 2.0 ltr Grand Vitara Keyless utafurahi sana.....
Pia hyo ya chini sio mbaya ila zina kasoro ya kutohandle speed kubwa pia nyingi zinakuwa sio economic hata kama ni ya 2.0 ltr sababu kuu ya kutokuwa economic ni kwamba zina gearbox yenye Overdrive iliyokuwa ya zamani....zina tabia ya kuhama barabara kiasi fulani, na ukipata yenye ulaji mzuri wa mafuta itakuwa gharama kubwa ambayo ukiongeza kidogo tu unapata hyo ya juu ambayo tunaiita TANAPA kwa arusha....ziko makini sana
Nakushauri uchukue ile kama kwenye picha kwanza pale juu maana ilitoka baada ya kujua makosa ya hyo ya chini na kuendana na soko la dunia ya sasa....