Naomba kujua kuhusu VAT ninapouza bidhaa

Fadhili10

New Member
Joined
Dec 26, 2019
Posts
2
Reaction score
1
Je, ninapouza bidhaa kwa mfano simu au laptpop, nitatoa risiti ambayo atapewa mteja, je mteja bei ninayomtajia mteja niunganishe na VAT humohumo au wadau mnafanyaje?
 
Ndo maana niliwashauri TRA, kuanzisha semina za kodi, kila mtu anayepata TIN/Kufungua biashara auhudhurie semina angalau ya siku moja kujua vitu basic kabla ya kukabidhiwa leseni.

Mzee nina uhakika hapo unafonya biashara kuna wafanyabiashara wengine pia. Hebu waulize wakuelekeze wao wanafanyaje. Maana unahitaji kujua elimu kuhusu mfumo mzima wa kodi za Tanzania, pamoja na kuweka kumbukumbu za hesabu zako ili mwisho wa siku mkono wa chuma usikuangukie
 
Ili uwe sawa siku zote, hesabu za biashara zako piga kabla ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) hii inalipwa na mlaji wa mwisho na ni ya serikali, wewe unapokea kwa niaba ya serikali, hivo chukua bei ya bidhaa kisha ongeza 18%. Lasivyo utaingia hasara mkuu.

Ndio maana sehemu zingine ukinunua bidhaa bila risiti bei inakuwa chini.

Kumbuka kila unapouza utoe risiti.


Nb. Hiyo hapo juu ina fanya kazi kama umeandikishwa na VRN.

Angalia kwenye risiti unazotoa kwenye mashine VAT inasoma kiasi gani, kwa ambao hawaunganishwa na VRN hutakiwi kuongeza 18%. Kwani unauza kwa bei halisi.

Kwa kuwa sahihi tafuta mshauri wa kodi atakusaidia zaidi. Me nimeeleza kwa uelewa wangu wa kawaida.
 
Je, ninapouza bidhaa kwa mfano simu au laptpop, nitatoa risiti ambayo atapewa mteja, je mteja bei ninayomtajia mteja niunganishe na VAT humohumo au wadau mnafanyaje?
Kwanza tuanzie hapa, je una sifa za kutoza VAT? kwani sio kila mfanya biashara ana sifa hizo, na kama una sifa hizo lazima utakuwa na certificate toka TRA, inayokutambulisha. kama unayo bei zako zote za bidhaa lazima zijumuishe kodi ya ongezeko la thamani(VAT) na kama unatumia mashine za EFD, hicho kiwango cha VAT, kitaonyeshwa hapo kwenye risiti na hicho ni mali ya TRA, kwani wewe unaikusanya kwa niaba yao!!
 
Je una VRN, yaani Vat Registration Number?, ili umtoze mteja VAT ni lazima uwe Vat registered otherwise huruhusiwi kumtoza mteja Vat kwani hutoweza kuisubmit TRA,so utakua umemuibia mteja na serikali.

Masharti au vigezo mojawapo ili uwe Vat registered ni lazima uwe na mauzo/turnover kuanzia million 100 per year or million 50 per half a year(6 months). Pia unaweza tembelea TRA kwa elimu zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Financial services
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimejifunza kitu.. thanks dear

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengi sana pamoja na baadhi ya tra inawapa maluelue VAT



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Upo sahihi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…