Naomba kujua kwanini Special Economic Zones (SEZ) hazijengwi nyingine mikoani?

Naomba kujua kwanini Special Economic Zones (SEZ) hazijengwi nyingine mikoani?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Kwa Tanzania, Export processing zones authority(EPZA) ndiyo husimamia na kuendesha hizi (SEZ) special economic zones.

Haya ni maeneo ambayo bidhaa huzalishwa kwaajili ya kuuza nje ya nchi. Mara nyingi huwa kunakuwa na punguzo kubwa la tozo. Mtu anaaigiza mashine na malighafi za viwandani bila tozo, na hiyo EPZA ndiyo inafuatilia uagizaji nk.

Hizi ni nzuri sana kwasababu hupunguza gharama za uzalishaji na kufanya bidhaa zetu kuweza kushindana.

Kwa Tanzania ni pale Mabibo tu, na kulikuwa na mpango wa kujenga nyingine maeneo ya Moro mjini.

Nataka kujua manufaa ya ile ya Mabibo na vitu ambavyo wanazalisha mpaka sasa. Hivi wanazalisha palepale?

Pia, kwanini hazianzishwi zingine mikoani, hasa mikoa ya mipakani kama Kagera, Mbeya, Songwe, Kigoma, Arusha, Ruvuma etc? Sio kwamba huko ndiyo zingekuwa na manufaa sana.
 
Back
Top Bottom