Naomba kujua mambo yakuzingatia kwenye biashara ya mtumba

Naomba kujua mambo yakuzingatia kwenye biashara ya mtumba

Mimi nakushauri fanya research kabla yakufanya hiyo bihashara ya mitumba mwanzo mgumu ila ukitulia utafanikiwa nimefanya hii bihashara kwamuda sasa , kama utapenda ushauri zaidi unaweza kupitia hapa Makumbusho stand kwenye maduka ya mitumba
 
Kiborondo
Mtaji wa 2m ni kidogo sana kwa aina ya Biashara unayotaka kufanya
Hyo 2m ukinunua Blouse za 5000 ilii uuze 7000/10000-15000
Unapata just 400 ambazo ni chache sana hata nusu ya upande wa Frame hazijai
Location: Mbagala sio Prime Location kwa aina hyo ya quality unayotaka.
Best location kwa Grade 1 ni Mwenge/ Makumbusho/ Kinondoni
Mbagala Market segment ni Low Class na Middle class , ukisema umuuzie Blouse kwa 10/15,000 utaishia kupata masonyo au zijaribiwe bila kununuliwa Mpaka upate Mtumba wa Mbagala kwa kujaa jasho na Make up za Mbagala Rangi 3.
Huo mtaji wa 2m usichukue hata Frame , labda upange kwenye ukuta wa Mtu na kodi isizidi 4,000/= TZS kwa Mwezi
Kama umependa ushauri wangu sema ambapo hujaelewa na uulize maswali zaidi
Umempa ushauri mzuri na ukweli kbs
 
Back
Top Bottom