Maneno,
Hapa tunajadili yale yaliyotokea Tanganyika.
Ukifananisha na yalitotokea kwengine tunakuwa tumetoka katika mjadala wetu.
La unataka tujadili yale yaliyofanywa na Wajerumani Namibia au hata Poland fungua uzi mpya nitakuja In Shaa Allah.
Sikiliza mkuu tatizo la mchango wako ume base sana katika uarabu na uislam na mimi nakuambia kuwa sioni kama ni busara na wazo zuri kufanya hivyo.
Ndiyo inawezekana kuwa kweli Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika na kusoma kiarabu na vile vile walikuwa wameelimika katika mambo ya mahesabu, sawa hata mimi nakubaliana na hilo, lakini sio katika herufi za kirumi kama ulivyosema. Lakini hata hivyo naomba utambue kuwa ni wazungu wote na sio wajerumani tu ndiyo walio tenda vitendo hivyo ulivyo visema vya kuwaona watu walio watawala ni wajinga na watu ambao hawajastaaribika, lengo lao hapa lilikuwa moja tu, total defamation and intimidation ili kufuta kila kitu ambacho sisi tulikuwa nacho na kukijua.
Kwote wazungu waliko kwenda hawakuyakuta manyani na masokwe, bali waliwakuta watu ambao wana cultures zao na maisha ambayo yalikuwa well organised. Hawakuwakuta wale walio kuwa wanaweza kusoma na kuandika kiarabu tu peke yao bali hata wale ambao hawakuwa na uwezo wa kusoma na kuandika kiarabu na kupiga mahesabu. Huwezi ukaniambia kwamba Tanganyika yote ilikuwa na watu ambao walikuwa wana uwezo wa kuandika na kusoma kiarabu na kufanya mahesabu tu?
Jibu ni hapana. Wakoloni wote waliüo vamia nchi za kiafrika na Amerika walihakikisha wanavuruga kila kitu ili wao wajiweke kwenye position ya kuwa rulers na sisi kwenye position ya watawaliwa. Ustaarabu wetu haukufaa tena na wala haukuwa kitu.
Kitu kingine ambacho ningependa ukifahamu ni kwamba, kustaarabika sio tu kuishi maisha ya kizungu au kiarabu, bali ni kitendo cha wanajamii kuishi kwa amani na kuweza kuwasiliana, kubadilishana mawazo na kuheshimiana baina yao na clans au makabila mengine bila kufanyiana vitendo vya kinyama vya kuuana ovyo, kama wazungu walivyo fanya baina yao kabla ya Berlin coference mwaka 1884 na baada ya mwaka 1914 ya World War 1.
Ustaarabu sio tu kujua kiarabu na uislam bali ni mwenendo mzima wa binadam kuishi katika amani na mpangilio mzuri wa kuendesha maisha yao katika kijamii.
Ukiuangalia mlolongo mzima wa maisha ya waarabu na uislam wao unao usifu utaona na kutatambua kuwa hata wao hawakuwa wasataarabu ki hivyo kama unavyo dhani au kuamini, kwani nao hawakuja kwetu Tanganyika kwa nia njema bali walikuja kwa mission. Walitusulubu sana sisi waafrika na kutufanya kuwa watumwa wao. Naona kwenye hii part umeisahau, nafikiri!
Zaidi ya hayo nakuomba chukua time kuiangalia hii documentary ili ujifunze zaidi jinsi gani Mnegro alivyo weza leta maendeleo ya kweli duniani ambayo wewe hivi sasa unayaona kama ni ustaarabu ulio letwa na waarabu na uislam wao au Caucasians na ukristo wao.
Na plaese, achana na historia za kupumbaza akili ulizo zisoma kwenye vitabu vilivyo andikwa na Caucasians, hiyo ni historia fake. Hiyo ni historia ambayo wao wali dictate mambo gani mazuri wayaandike na mambo gani wasiyaandike. Wapindisha historia lwa kadri walibyo ona inawafaa wao.
Mwisho naomba utambue pia kuwa Mwarabu sio Mmisri na wala sio Mnegro bali ni mtu mwenye asili ya ki-Caucasian!