Naomba kujua Nyumba zinazonukia, Wanafanyaje?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Kuna nyumba niliingia hivi karibuni dah ilikuwa ina nukia harufu nzuri ajabu

Nimejikuta niko curious na nini hasa wanatumia hadi nyumba inanukia vile

Nilishindwa kuuliza sababu kilichonipeleka kilikuwa kingine kabisa

Wenye tips za kuwezesha nyumba zetu zinukie hebu wekeni hapa

Ni nini hasa mnatumia?
 
Mimi kwangu huwa natumia air fresheners za kuchomeka kwenye soketi za umeme na ambazo ninaweza kudhibiti kiasi cha marashi yatokayo.

Baadaye nitaweka picha hapa muone nachozungumzia.

Jingine ni kutumia scented candles. Napendelea zaidi brand ya Yankee Candle.

Na huwa sipendi kupika vyakula vyenye shombo kali kama vile kukaanga samaki na kadhalika.

Nikikaanga samaki huwa nakaangia nje kwenye deck.

Halafu huwa napendelea zaidi marashi ya fresh na citrus.

Usafi wa nyumba nao husaidia pia. Hakikisha nyumba yako ni safi na yenye kuingiza na kutoa hewa vizuri.
 


picha itasaidia
 


Wanafukiza amma udi (oud) amma perfume.

Zipo perfumes na vitezo vyake za kufukiza. (google "perfume burners").
 
Kumbe na huko "Maobama" kuna samaki wenye shombo kama kwetu Musoma-Mara?
 
Candles za flavor tofauti zinasaidia
 


Msukuma na air-freshener wapi na wapi, wacha uongo.
 
We jamaa bhana..yaani umeshindwa kuniuliza pale pale home mpaka uje JF!?

Anyways Mimi njia yangu ni simple saana, natumia njia natural and sustainable nimepanda maua madogo mazuri halisi kabisa pale sebuleni na baadhi ya maeneo ndani kwenye vikopo maalumu..maua hayo ni special kwa ajili ya home aromas..maua yanapatikana Spain, Italy and Turkey mostly yanaitwa Queen of the aromatic night...!

Ukija tena uniambie nikukatie kaua ukapande home kamche kamoja tu kanatosha kunukisha hata ghorofa. In case usiponikuta we chuma kajani kamoja kwa kuvizia akikisha mlinzi hakuoni maana hanaga dogo yule yero!
 

kuna nyumba unakuta inanukia
mtu mwenyewe ananukia
gari yake inanukia

yaani dah
 
Hahaha...Sorry, this is funny man.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…