Naomba kujua tafsiri sahihi ya mmachinga ambaye ndie mlengwa wa kitambulisho cha umachinga

mfuga kuku

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2014
Posts
824
Reaction score
650
Habari za muda huu wana jukwaa! Naomba kujua tafsiri sahihi ya mmachinga ambae ndie mlengwa wa kitambulisho cha umachinga!

Swali langu: kama wewe ni mtumishi wa serikali mfano mwalim, au muhudumu wa ofisi, una kakibanda kako maeneo ya mjini Unauza uza pipi, sigara, vocha na vitu vingine vidogo vidogo, je ukienda kuchukua kitambulisho kile ni Makosa kisheria?
 
Ndiyo wewe unatakiwa uwe na tin number wewe Sio machinga kwa sababu unakibanda
Acha uzembe nenda tra wakupe tin number
Lipa kodi kwa maendeleo ya nchi
Kaka kakibanda cha bati, mauzo sh 2500/= kwa siku ndio nikachukue tin namba?
 
Sio kosa cha msingi in mauzo/faida yako yasizidi million nne kwa mwaka
 
Kajaribu kwenda mkuu halafu usiache kuleta mrejesho hapa.

Wajuzi watakujuza mkuu lakin
Nitaleta mrejesho Ndg! Inawezekana wengi Wapo kama mm NA tunaogopa kwenda kuchukua vitambulisho hivi.
 
Kaka kakibanda cha bati, mauzo sh 2500/= kwa siku ndio nikachukue tin namba?
Kuwa mkweli dhamiri yako ikukushudia
Je unauza 2500 tuu kwa Siku??
Unajua tatizo wabongo ni waongo usikwepe kodi
Ndiyo maana inabidi serikali iweke fixed amount kwa watu kama ninyi mnao Ongea uongo
 
Kuwa mkweli dhamiri yako ikukushudia
Je unauza 2500 tuu kwa Siku??
Unajua tatizo wabongo ni waongo usikwepe kodi
Ndiyo maana inabidi serikali iweke fixed amount kwa watu kama ninyi mnao Ongea uongo
Ama kweli alieshiba hamjui mwenye njaa! Hapa hata ukimwambia mtu kama naishi kwa mlo mmoja kwa siku mtu hawezi kuamini!
 
Najua mauzo ila inatolewa kwenye faida
Mkuu kodi, hutozwa kwenye mauzo ghafi, ndio maana, hata jedwari la viwango vya kodi la TRA, wame group kwa kiwango cha mauzo. Na hata siku moja watakuulizi kiwango cha faida. Ila kwa wenye mauzo nadhani kuanzia milioni 140 kwa mwaka, ndio wana kuwa na sifa za kutoza VAT. wao ndio yanachukuliwa mauzo ghafi, wanatoa manunuzi yaliyofanyika mwezi husika, ile tofauti ndio unalipa/una rejeshewa. Lakini hakuna kodi inayo tozwa kwenye faida, kwani ingekuwa ni ngumu sana kwa serikali kupata kodi, kila mtu angefanya matumizi yakawa makubwa kuliko mauzo,
 
Alisema biashara yoyote chini ya milioni nne una haki ya kuchukuwa kitambulisho hata kama unakibada
Ndiyo wewe unatakiwa uwe na tin number wewe Sio machinga kwa sababu unakibanda
Acha uzembe nenda tra wakupe tin number
Lipa kodi kwa maendeleo ya nchi
 
samahani ndugu unafanya biashara gani?
Nauza pipi, biscuit, viberiti, maji safi ya kunywa, pop cone, vyote hivyo ni reja reja! Ukifika jioni nahamisha bidhaa zangu kwa hofu ya kuibiwa, kesho asbh napanga tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…