Naomba kujua tofauti ya Rappers na Mcee ni ipi?

Naomba kujua tofauti ya Rappers na Mcee ni ipi?

Emcee ni yeyote anayetumia kinywa chake kuwarusha watu (moving the crowd), hata DJ anaweza kuwa emcee.

Emcee hufikiri kabla ya kusema. Rappers mara nyingi huwa ni wanasema tu hata kama havina maana, mradi vibes. Mfano mzuri ni Jay Mo anafikiri kabla ya kusema, Godzilla alikuwa anasema tu.

Rappers wao huangalia hela na umaarufu zaidi na ikibidi hata kukosa adabu na kujivunjia heshima, while emcees huangalia heshima zaidi.
 
Hii mada ilishawahi kuletwa humu na nilijibu hivi

Unapoongelea elements za MC unatakiwa uelewe kwamba ni lazima awe na uwezo wa kuwakilisha jamii

MC anatakiwa awe na uwezo wa kuwakilisha, kuwasilisha na kufikisha taarifa kwa jamii. Na pia anaweza akawa na vinasaba vya upande wa biashara

Jambo ambalo wengi wanashindwa kuelewa ni kua MC ni rapper pia lakini utofauti kati ya MC na rapper ni kwamba rapper mara nyingi huongea kuhusu personal issues.

Mfano mzuri kama madee "nani kamwaga pombe yangu" au young killer "sina swaga" nk. Unaona kabisa kua hivyo ni vitu ambavyo vinamuhusu yeye

MC sasa tukichukulia mfano wa mtu kama Professa j na mtu kama fid q unaweza ukaaona ni watu wenye uwezo wa kuelezea mambo ya kukufundisha, haimuhusu yeye tu bali jamii kiujumla

MC huongea kama mtu wa tatu anapo delivery ujumbe wake. Mfano wa mzuri ni hii verse ya fid Q "ongea maisha ya kuunga unga hii shuhuli mi naiweza, hapa utaambulia ushauri tu ukihitaji msaada wa kifedha.../"
Mc ni kama 2pac na rapper ni BIG Notorious

Mc ni kama Rakim
Ni kam Talib Kweli
Ni kama Lupe Fiasco
Ni kama Kendrick Lamar
 
Back
Top Bottom