Hii mada ilishawahi kuletwa humu na nilijibu hivi
Unapoongelea elements za MC unatakiwa uelewe kwamba ni lazima awe na uwezo wa kuwakilisha jamii
MC anatakiwa awe na uwezo wa kuwakilisha, kuwasilisha na kufikisha taarifa kwa jamii. Na pia anaweza akawa na vinasaba vya upande wa biashara
Jambo ambalo wengi wanashindwa kuelewa ni kua MC ni rapper pia lakini utofauti kati ya MC na rapper ni kwamba rapper mara nyingi huongea kuhusu personal issues.
Mfano mzuri kama madee "nani kamwaga pombe yangu" au young killer "sina swaga" nk. Unaona kabisa kua hivyo ni vitu ambavyo vinamuhusu yeye
MC sasa tukichukulia mfano wa mtu kama Professa j na mtu kama fid q unaweza ukaaona ni watu wenye uwezo wa kuelezea mambo ya kukufundisha, haimuhusu yeye tu bali jamii kiujumla
MC huongea kama mtu wa tatu anapo delivery ujumbe wake. Mfano wa mzuri ni hii verse ya fid Q "ongea maisha ya kuunga unga hii shuhuli mi naiweza, hapa utaambulia ushauri tu ukihitaji msaada wa kifedha.../"