Naomba kujua uwezo wa Suzuki Carry (Minivan)

Naomba kujua uwezo wa Suzuki Carry (Minivan)

DREAMBOY

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
2,117
Reaction score
1,369
1596446831069.png

Suzuki Carry

Habari zenu!

Naomba kujulishwa uwezo wa suzuki carry a.k.a kirikuu:

1. Uwezo wa kubeba(maximum weight).

2. Nguvu yake kwenye mchanga,matope,utelezi,miinuko n.k. (pulling).

3. Je inaweza rough roads hasa mikoa isiyokuwa na milima mikali au maeneo yenye miinuko ya wastani.

4. Upatikanaji wa spares.

5. Generation zake na ubora wa kila uzao?

Na mengine mengi.

Asanteni!
 
Jamani wana jukwaa, tupeni basi moja mbili kuhusu hivyo vigari, nyie kila siku alteza alteza
Nami nasubiri kwa hamu bila shaka sidhan kama wataniangusha.
 
Kigari ambacho hakipendi shida. Kina piston tatu kama akina Passo (aka pasua). Kina beba kilo 350 lakini kibongobongo wanakibebesha zaidi. Uzito ukizidi engine inakufa.

Engine yake ni delicate kiasi huwezi ifanyia overhaul halafu huuzwa bei sawa na ist and the like. Mafundi gereji wanakikimbia sana kutokana na komplext zake. Kinaweza pata miss kiasi cha kutorekebishika.

Vikianza tatizo la kuchemsha ndio basi. Mara nyingi mafundi hufunga fan direct kikianza kukorofisha. Mi changu kiko garage mpaka sasa fundi anahangaika nacho.
 
Kigari ambacho hakipendi shida. Kina piston tatu kama akina Passo (aka pasua). Kina beba kilo 350 lakini kibongobongo wanakibebesha zaidi. Uzito ukizidi engine inakufa...
Kaka nasikia vipo generations nyingi, nisaidie nasikia vpo vinavyobeba tani moja
 
Kigari ambacho hakipendi shida. Kina piston tatu kama akina Passo (aka pasua). Kina beba kilo 350 lakini kibongobongo wanakibebesha zaidi. Uzito ukizidi engine inakufa...
Shida inaanzia kwenye driving ya hivi Vigari, ukishakuwa loaded accelerate very very gentle , hii husaidia kutolundika mafuta mengi kwenye cylinders

rich mixture husababisha liquid hammering kwenye cylinders ,na kwa kweli hzi gari zina cylinder delicate sana, zikitanuka au kupata michubuko huwa hazitulii tena. UKIWEZA kuendesha vizuri ukafatilia na service ya oil nzuri, kitadumu.
 
Shida inaanzia kwenye driving ya hivi Vigari, ukishakuwa loaded accelerate very very gentle , hii husaidia kutolundika mafuta mengi kwenye cylinders

rich mixture husababisha liquid hammering kwenye cylinders ,na kwa kweli hzi gari zina cylinder delicate sana, zikitanuka au kupata michubuko huwa hazitulii tena
UKIWEZA kuendesha vizuri ukafatilia na service ya oil nzuri, kitadumu.
Lugha ya kiufundi ni ngumu.
 
Kigari ambacho hakipendi shida. Kina piston tatu kama akina Passo (aka pasua). Kina beba kilo 350 lakini kibongobongo wanakibebesha zaidi. Uzito ukizidi engine inakufa. ...
Mkuu mimi kuna mchawi wa hivi vidude namjua, huyu jamaa ni balaa, kama fundi wako kachemka nistue pm(thank me later)
 
Back
Top Bottom