Ni vitabu vya kubuni juu ya mambo/ uwezo wa sayansi. Mfano kimoja kilisimulia habari ya mtu mmoja mzee tajiri aliyeona mwili umechoka akachukua akili yake na kuipachika kwenye mwili wa kijana na yule kijana kupewa mwili wa kizee. Zingine zinazungumzia ndege/meli zinazoweza kusafiri kwenye sayari za mbali.
Hata hii safari ya kwenda Mars ilianza kama Science fiction. Hata safari ya mwezini ilianza hivyo. Ina mambo mengi sana. Lakini kubwa ni kuonyesha safari ya kufikirika.