Nachanganya vipi au nawekaje kwenye mchuzi.
Je hiyo vitunguu saum imesagwa au nahitaji kuponda ponda kwenye kakinu kadogo?
Aisee kuandika itakua mtihani ila ngoja nijaribu,
Nyama yako ikiwa mbichi ioshe vizuri, weka chumvi, limao, Tangawizi au Thom au vyote (i prefer thom pekee)
weka jikoni ichemke hadi iive, wakati unasubiri nyama iive anza kuandaa viungo,
Kitunguu,
Nyanya, (unaweza kusaga au ukakata tu)
Karoti, (unaweza kusaga au ukakata tu)
Hoho,
Thom iliyopondwa kwa kinu(inakua fresh) ni bora kuliko ya unga.
Ninavyopika sasa hehehe culture gal akiwa jikoni kama najiona vile.... lol.
Nyama ikiwa haina mifupa wala huna haja ya kubadili sufuria, weka mafuta kidogo sana kama haina mafuta nyama,
Tupia kitungua maji kaanga kiasi hua sipendi ule utaratibu mpk kiwe cha brown,
tupia karot, hoho na thom.... endelea kukaanga nyama na viungo vyako kiasi kisha weka nyanya pmj na unga wa Curry powder kama kijiko kimoja cha chai au viwili kutegemea na upendavyo, tupia na unga wa birian masala kama nusu kijiko cha chai hivi kuongezea ladha.... endelea kukaanga mpk nyanya ziive, (nyanya ziache mpk zianze kushika chini maana ukiwahi kuongeza maji zitakua bado mbichi na kuharibu ladha ya mchuzi wako)
Tupia pilipili kama ni mpenzi kama sio waweza kuacha maana hata curry ina ladha ya pilipili kwa mbaali.
Utaweka maji kiasi ni vema kuacha mchuzi mzito kuliko chururu kama wa kipemba (lol am sorry wapemba).
kisha epua mchuzi wako tayari kwa kuliwa iwe chapati, wali, maandazi, tambi au ugali.
Same procedure na samaki.