Naomba kujua viungo tofauti vya kuweka kwenye nyama au samaki

Naomba kujua viungo tofauti vya kuweka kwenye nyama au samaki

Viungo vizuri vya kuweka kwenye mchuzi wa nyama au samaki ni;
Hoho
Karoti
Vitunguu {Thomu + maji}
Tangawizi
Uzile {binzari nyembamba}
Hiliki
Mdalasini
Au ukipata pilau + biriani masala ni vizuri zaidi.

Naogopa kukukaribisha kwangu utakuwa huondoki wewe
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 
Aisee kuandika itakua mtihani ila ngoja nijaribu,
Nyama yako ikiwa mbichi ioshe vizuri, weka chumvi, limao, Tangawizi au Thom au vyote (i prefer thom pekee)
weka jikoni ichemke hadi iive, wakati unasubiri nyama iive anza kuandaa viungo,
Kitunguu,
Nyanya, (unaweza kusaga au ukakata tu)
Karoti, (unaweza kusaga au ukakata tu)
Hoho,
Thom iliyopondwa kwa kinu(inakua fresh) ni bora kuliko ya unga.

Ninavyopika sasa hehehe culture gal akiwa jikoni kama najiona vile.... lol.

Nyama ikiwa haina mifupa wala huna haja ya kubadili sufuria, weka mafuta kidogo sana kama haina mafuta nyama,
Tupia kitungua maji kaanga kiasi hua sipendi ule utaratibu mpk kiwe cha brown,
tupia karot, hoho na thom.... endelea kukaanga nyama na viungo vyako kiasi kisha weka nyanya pmj na unga wa Curry powder kama kijiko kimoja cha chai au viwili kutegemea na upendavyo, tupia na unga wa birian masala kama nusu kijiko cha chai hivi kuongezea ladha.... endelea kukaanga mpk nyanya ziive, (nyanya ziache mpk zianze kushika chini maana ukiwahi kuongeza maji zitakua bado mbichi na kuharibu ladha ya mchuzi wako)

Tupia pilipili kama ni mpenzi kama sio waweza kuacha maana hata curry ina ladha ya pilipili kwa mbaali.

Utaweka maji kiasi ni vema kuacha mchuzi mzito kuliko chururu kama wa kipemba (lol am sorry wapemba).

kisha epua mchuzi wako tayari kwa kuliwa iwe chapati, wali, maandazi, tambi au ugali.

Same procedure na samaki.
Yaani wewe ukinikuta nipo jikoni utakimbia wewe[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 
Yaani wewe ukinikuta nipo jikoni utakimbia wewe[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
Lol, unapika bila nguo nini?? hahaha
 
Nunua Curry powder ile ya Zanzibar masala ukiweka na Birian masala (ya zanzibar) kidoogo weee mbona utang'ata vidole.

Aisee mchuzi bila curry powder na thom (vitunguu saum) hua haupandi kabisaaa nitajilazimisha tu.
Weka picha plse
 
Kama unataka kuifanya kwa huku bara sio mbaya, nenda kanunue viungo vyote kuanzia kilo, then uje ufunge kwenye ile mifuko, kwa bei ya 500 tu kwa kimfuko, vinalipa.
Santeeeee, ngoja nifanye hivyo aiseee naitafutia package nzuuuuri.
 
Habari ya wakati huu.

Wakuu, najifunza kupika baada ya kuamua kupunguza kula migahawani.

Naomba kujua viungo au namna tofauti tofauti za kupika nyama au samaki. Namaaniaha viungo vya kuweka kwenye mchuzi wa nyama iwe nzuri zaidi.

Najua kupika nyama ile kawaida, kuweka nyanya, karoti, pilipili hoho, kitunguu na chumvi. Ila hua nakula migahawani nyama inanukia vizuri na inaladha nzuri, naambiwa umewekewa viungo tofauti tofauti.

Naomba kufundishwa au kuelekezwa viungo vya kupikia nyama au samaki.

Ahsanteni sana.

Uwekaji wa viungo ktk nyama na samaki kunategemea na namna upishi wa hicho chakula. Labda ungetueleza unataka hivyo viungo kwa ajili ya upishi upi wa samaki au nyama
 
Back
Top Bottom