Naomba kujulishwa kuhusu malori ya HOWO

jembelamkono

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Posts
2,733
Reaction score
2,012
Habari wakuu,

Naomba mwenye uelewa juu ya hizi malori ya kichina! HOWO kuhusu agent wake kwa hapa Tanzania (Brand new)! Ubora kulinganisha na scania, DAF, Mercedes. Bei, Service n.k anijuze hapa tafadhali.

Siyo mbaya kama atagusia pia na aina za trella na bei zake.

Wasalaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda barabara ya nyerere kuanzia Vingunguti hadi kipawa huwezi kosa. Au nenda Big brother pale mabibo utawakuta.

Tractor 3 za Howo zinanunua Tractor 1 ya Scania au M/ Benz

Kwa equivalent hiyo unaweza kutafuta Ubora wa howo.

Ni ka kama hesabu za vibox tuu

Siyakudumisa Thixo
 
Vizuri mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Jembe la mkono ulichotakiwa kuuliza ni Howo tuu sasa ukitaka kufananisha ubora sijui na Scania au Mercedes Benz maana huyo Scania kwa ubora hamfikii mbali sana Mercedes Benz sio kwa ukaribu anaeweza kumkaribia ni Man Diesel...Howo pia ukipata Mpya sio mbaya kwa kuanzia mpaka ikianza kusumbua na inachukua muda itakua imefanya kazi..
 
Hizi gari ,RDC zipo nyingi sana, zinapiga kazi migodini kubeba mineral ore ,za 40 tonnes



MTC | 101| [emoji769]
 
howo utaipenda ikiwa bado mpya haijaanza shida ,ila zikianza kusumbua kama kufanyia engine overhaul mara nyingi zinakuwa zinakataa ndio maana wenye kujiweza huwa wanafunga mashine mpya tofauti na scania au benz ukipiga overhaul inakuwa jiwe kweli , kiufupi howo ni gari ya biashara scania ni gari ya kazi au kama unazijua iveco euro
kwa wakala wa hizo howo naonaga pale tazara jirani na sophia house
 
Shukrani kwa mchango wako mkuu,je unaweza kujua bei ya horse mpya ya Howo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…