Naomba kujuzwa bei ya Spark Plug

Kweli kabisaa mkuu,ila watu hua wanaweka mpk brake pad used hapo ndio hua wananichanganya zaidi.
Na hao ndio wanaongoza kuuliza bei ukimwambia kiasi hiki genuine na mpya atakuuliza na used yake bei gani sasa unabak unamshangaa unapenda used wakati aliyekuwa anaitumia kaichoka utaitumiaje na unaweza kukuta used na mpya zinatofautiana kidog tu lkn kwa sababu wameshakalilishwa used basi yeye ni kuchukua tu
 
Mrejesho: Nmefanikiwa kubadili plug zote nne kwa bei ya 25,000 kila plug. Jumla kuu 100,000/= Nmenunua Denso baada ya fundi kuniambia kuwa zinaendana na gari yangu (Suzuki swift 2002).

Baada ya kubadili plug gari inachanganya vizuri tofauti na zamani. Nmenunua bush pamoja na kuzifunga.
Bei ya bush 6 ni 180,000/=

Natakiwa kununua shock up mpya 4 kila moja 130,000/=.

Spare genuine ni ghali ila zinadumu sana.
 
Kwenye shockup hapo hizo unazonunua sio genuine mkuu hizo ni from China genuine shockup kwa hizo 4 ulitakiwa kulipia kama milioni 3 kasoro
 
Plug umenunua za madini gani...?
Platinum, Iridium au Copper...?
Na je ni zile za sindano au za kawaida...

Denso, NGK, Bosch are all ok...
 
Siku watu wakijua umuhimu wa vifaa vya magari yao nadhan wataachana na hii kasumba ya kununua vitu fake genuine spark plug ya Toyota bei inaanzia 15000 hapa kutegemeana na aina ya plug chini ya hapo hakuna plug hapo
Sure, mi nimeenda Kwa dealer wa Toyota kaniuzia moja 15000 ni NGK. Wakasema nikitaka zinazokaa muda mrefu za iridium bei imesimama sana ila wao wameishiwa. Mimi vitu vinavyohusu engine nafunga original

Sent from my Nokia 6.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mi spea ya engine lazima nipate og tena ile ambayo ni bora kabisa sokoni kwa wakati huo. Vitu feki nitafunga labda shokap

Sent from my Nokia 6.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Shokap ni mchina. Nikienda toyota shop, nilitajiwa bei ya shokap mbili za mbele ni sh.1300,000/=. Maana yake shokap 1 ni 650K. Kwa mantiki hiyo hizo shokap ulizonunua sio og mkuu.

Sent from my Nokia 6.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kwenye shockup hapo hizo unazonunua sio genuine mkuu hizo ni from China genuine shockup kwa hizo 4 ulitakiwa kulipia kama milioni 3 kasoro
Ni kweli mimi huwa nanunua spea kwa toyota branch Tz, shokap za gari yangu ndogo nilitajiwa moja sh.650,000. So, upo sahihi kabisa

Sent from my Nokia 6.1 Plus using JamiiForums mobile app
 

Sure,nissan pale master card ni 30K
 
Kweli kabisaa mkuu, ila watu hua wanaweka mpk brake pad used hapo ndio hua wananichanganya zaidi.
Brake pad unawekaje used sasa?🤣🤣🤣 Itoshe kusema kuwa vitu used ni kipengele jamani. Ambacho naeza weka used kwenye gari yangu ni matairi tu ambayo still nayanunua nusu ya bei ya tairi mpya maana kwangu sioni tofauti kwa ubora wa tyre mpya na used as long as mpira ni mzima na kashata bado mbichi! Hela ya tairi moja mpya naweza pata used tyres mbili ambazo ziko Order sana sababu mkoa niliopo vipuri vya gari bei ni kichaa.
 

'Ambacho naeza weka used kwenye gari yangu ni matairi tu'.

Hahah sasa hapo ndipo tunatofautiana mzee baba,tyre used siigusi hata kwa dawa niko so sensitive yaani hapo lazima nikamenye kitu kipyaa dukani.

Kwa hio mzee baba shock ups za gari yako(kama ni toyota) unaendaga kununua hizo za Tsh.650,000 per shock up sio?

Shock up za gari yangu hua naagiza za KYB brand ni za ukweli kinyamaaaa.
 
Mie mipira napointi kwa sasa mwanzo nilinunua piru ila nikaona najila sana. Maana sioni tofauti kabisa ya kiatu used na kipya.

Braza, gari yangu naipenda ila kimsingi siwezi nunua shockup 650k!!! Hizo mbanga zinawahusu wale wa Nissan brand. Sikutaka hizo tabu na ndio maana nilichagua gari economical kwangu.

Gas filled Durable shockup ni 85K kwa moja. Nikinunua pair nasahau!
 
Hivi utajuaje Plug imeshachoka kwenye gari yako hivyo upaswe kuweka mpya?
Fungua uzicheki, kwa magari mengi kazi ya kufungua plug ni rahisi sana. Dalili za kuchoka plug ni nyingi na pia zinafanana na dalili za magonjwa mengine ya gari. Dalili hizi ni kwa uchache ni misfire na gari kukosa nguvu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…