Naomba kujuzwa faida za kuwa na GREEN CARD ya Marekani

Naomba kujuzwa faida za kuwa na GREEN CARD ya Marekani

Wana familia wa JF,

Humu ndani naamini wapo Watanzania ambao wanaishi Marekani kwa nguvu ya GREEN CARD.

Kwa faida ya wengi, naomba yeyote anayejua au amefanikiwa kuwa na Green Card ya Marekani ni kwa namna gani imemsaidia kuishi huko USA na kwa namna gani imemsaidia kupata kazi nzuri na kuweza ku-make enough cash na kutimiza ndoto zake.

Pia naomba kufahamu changamoto ambayo mtu aliyeshinda Green Card anaweza kukutana nayo mara tu anaingia Marekani for the first time au nini afanye ili mambo yaende sawa.

Mwisho naomba kujua kama mtu akiacha mshahahara wa 3M Bongo akienda Marekani anaweza ku-make fedha ndefu zaidi na hasa akiwa na hayo makaratasi kwa maana ya Green Card au ndio inaweza kuwa anapotea kimaisha?

Natanguliza shukrani kwa wajuzi wa haya mambo na naamini mchango wenu utasaidia Watanzania wengi kufahamu kuhusu faida za kuwa na Green Card ya Marekani.

ASANTENI SANA 🙏🙏
Nenda YouTube search For EBMSWAHILI/EM SCHOOLERS kaeleza hajaacha kitu
 
Kama una mshahara wa 3m hapa TZ una chance kubwa ya kufanikiwa ukiwa hapahapa. Kwenda nchi za watu utapoteza miaka zaidi ya miwili kujitafuta na kufit kwenye mifumo yao. KOMAA HAPAHAPA
Mafanikio kwako ni nini?
 
Mkuu hakuna nchi nzuri duniani kama Tanzania blv or not...Tanzania ni nchi pekee ambayo kuna watu hawalali ili wananchi wake walale...sio kawaida kila siku unaamka unafanya shughuli zako salama..unarudi kwako salama tena kwa muda unaotaka...katika nchi ina uungwana Africa ni Tanzania.

Kwa Asia ni ni nchi nyingi wamejengewa ustarabu..:na heshima...South korea da best...America kama ukienda nenda kajifunze(exposure) then uje bongo ufanye investments...hii yanga mnayo iona sa hiv si bahat mbaya...yule Rais aisee IQ yake si ya kawaida nenden chuo flan hapo posta mkaulize taarifa zake.

He is not normal guy ever..,,na ametokea chin kabisaa..,njaa anaifaham, imagine b4 hajui kama atakuwa Rais...but kila mimba ya mtoto wake lazima wife akajifungulie America...very geniouz guy. Wewe unalipwa mil3 unataka ukimbilie USA usalama wako ni mdogo bna..
Kweli Tz ni nchi nzuri na ni nyumbani. Lakini nakuhakikishia kuna nchi zaidi ya 5 Afrika ambazo ni nzuri kuliko Tz na kuna nchi zaidi ya 20 duniani ambazo ni nzuri pia kuliko Tz.
 
Hakuna faida yoyote; unaruhusiwa kuishi na kufanya kazi bila kubugudhiwa tu lakini haina maana kuwa hiyo ni faida kwani inategemea na vigezo vingine vingi hadi uweze kuiita kuwa ni faida. Unaweza kuwa na green card, ukaishia kuishi kwenye trailer na kufanya kazi ya bora mkono wende kinywani tu.

Ukipata green card usijisahau ukadhani umepata faida sana
Inachukua muda gani kwa green card kuwa revoked kwa kutoshi Marekani tangu uipate
 
Kwa hela hiyo pambana mdogo mdogo within 5 years ifike angalau 5-10M bongo unaishi fresh tu kuliko huko.......

Marekani utapaona pazuri kama ukitokea class ya chini sababu hata kufanya manual work inakua sio ishu mpaka ujipate

Kwa hali yako uliyonayo kiuchumi utapata sonona ukienda huko, maisha ya marekani sahizi ni magumu na hayatotengemaa any time soon (uwe unaangalia market Mondays you tube and the likes) ukiwa mgeni ts even worse
 
Kama una mshahara wa 3m hapa TZ una chance kubwa ya kufanikiwa ukiwa hapahapa. Kwenda nchi za watu utapoteza miaka zaidi ya miwili kujitafuta na kufit kwenye mifumo yao. KOMAA HAPAHAPA
Uchumi wa US sahizi ni kisanga, angalu ukiwa mwenyeji you can maneuver yourself
Na kama hana mwanamke bado hajakutana na cultural shock ya dating environment

Ajikusanye apate visa hata ya mwezi akapime upepo
 
Inachukua muda gani kwa green card kuwa revoked kwa kutoshi Marekani tangu uipate
Ni miezi sita unless uwe na kibali maalum cha kukuruhusu kukaa nje ya marekani kwa zaidi ya miezi sita
 
Aisee kuna vitu vingi nimeokota hapa kwny huu uzi,Big up..
 
Ni miezi sita unless uwe na kibali maalum cha kukuruhusu kukaa nje ya marekani kwa zaidi ya miezi sita
Hapa ni pazuri sana unazikusanya us ,

unawaambia Wana wanakuandalia heka zako kumi mitaa ya njombe unaenda kulima kiazi Cha kumwagilia kuanzia wa Saba mwisho kufikia wa kumi mwishoni unavuna unalud zako us unaenda kuwatambia Wana jinsi ulivyo na harakati si mchezo wanadiaspora lazima waone wivu teheeeeeeee
 
Back
Top Bottom