Naomba kujuzwa gharama za kipimo cha DNA

Kuna habari nimesoma kwenye page ya maulid kitenge kwamba kuna mbaba huko Arusha ambaye mwanae ni mmoja wa wahanga wa tukio la vifo vya wale watoto wa shule ya Ghati memorial walio sombwa na maji wakafa.

Huyu baba kafika msibani anakuta jina la baba lililopo kwenye msalaba sio jina lake, kuuliza mkewe anamwambia yeye sio baba halisi wa mtoto.

Na muda wote mtoto akiwa hai yeye ndio alikuwa analea na kutoa huduma zote.
 
Ni laki moja mkuu kipimo! Ila fuata taratibu zote.
Hawa wanawake wanapenda kubambikia watoto hakuna kitu kinauma kama hicho! Kubambikiwa na baadae kuja kujua kuwa mtoto si wako.
Bora akuambie ukweli kuwa alitereza hapo ndio utaona mnafanyaje!

Hata wazungu nao hawapendi kubambikiwa. Hio ni dhambi sana wanawake hawajui tu. Alafu unakuta jamaa bado linamla na limemzalia..
Usitishiwe na kauli za watu humu kuwa kitanda sijui hakizai haramu.

Mwanamke hadi kufikia kuzaa na mwanaume mwingine ni Hatari sana hata maisha yako yanakua yapo ukingoni.
LISTEN TO YOUR HEART bado unasafari ndefu ya maisha.usifanye kitu kwa huruma na kuja kuumia baadae.
Asante sana mkuu
 
Kuna habari nimesoma kwenye page ya maulid kitenge kwamba kuna mbaba huko Arusha ambaye mwanae ni mmoja wa wahanga wa tukio la vifo vya wale watoto wa shule ya Ghati memorial walio sombwa na maji wakafa.

Huyu baba kafika msibani anakuta jina la baba lililopo kwenye msalaba sio jina lake, kuuliza mkewe anamwambia yeye sio baba halisi wa mtoto.

Na muda wote mtoto akiwa hai yeye ndio alikuwa analea na kutoa huduma zote.
Inaumiza sana😢😢
 
Ni laki moja mkuu kipimo! Ila fuata taratibu zote.
Hawa wanawake wanapenda kubambikia watoto hakuna kitu kinauma kama hicho! Kubambikiwa na baadae kuja kujua kuwa mtoto si wako.
Bora akuambie ukweli kuwa alitereza hapo ndio utaona mnafanyaje!

Hata wazungu nao hawapendi kubambikiwa. Hio ni dhambi sana wanawake hawajui tu. Alafu unakuta jamaa bado linamla na amemzalia..
Usitishiwe na kauli za watu humu kuwa kitanda sijui hakizai haramu.

Mwanamke hadi kufikia kuzaa na mwanaume mwingine ni Hatari sana hata maisha yako yanakua yapo ukingoni.
LISTEN TO YOUR HEART bado unasafari ndefu ya maisha.usifanye kitu kwa huruma na kuja kuumia baadae.
Aandae laki tatu na elfu hamsini hivi. Watatu Kila mmoja laki, elfu 50 nauli za kumsafirisha afisa kwenda kwa mkemia na mambo mengine madogo madogo
 
Wewe lea tu hata kama huyo mtoto unahisi siyo wa kwako. Utapata thawabu mbele za Mungu.
 
Achana nacho tu maana utapewa majibu ya huyo mtoto ni wako ata kama si kweli.
 
Ni kweli haipimwi kiholela tu, upo utaratibu wa kufuta.

DR Mambo Jambo
Huduma za uchunguzi wa vinasaba hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009.Taratibu zifuatazo hufuatwa ili kuweza kupata huduma za uchunguzi;-

1. Mteja anayehitaji kupatiwa huduma za uchunguzi wa Vinasaba anawakilishwa na taasisi zilizotajwa kwenye sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya Mwaka 2009 ili kumuombea mteja husika huduma za uchunguzi

2. Kwa mujibu wa kifungu cha 25(2) cha Sheria ya vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009, taasisi zinazoruhusiwa kumuombea mteja kupatiwa huduma za uchunguzi wa vinasabani pamoja na
  • Maafisa ustawi wa jamii
  • Mawakili
  • Mahakama katika uchunguzi unaolenga kutataua migogoro
  • Jeshi la polisi kwa masuala yanayohusu jinai
  • Madakatari kwa uchunguzi unaihusiana na tiba
  • Wakuu wa Wilaya
  • Taasisi za Tafiti zinazotambuliwa Kisheria
3. Taasisi hizo zitaandika barua za maombi ya kupatiwa huduma za uchunguzi kwa niaba ya mteja husika. Barua zote zitaandika kwenda kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali.

4. Malipo ya uchunguzi ni Tsh100, 000/=kwa sampuli ya mtu mmoja, hivyo kwa uchunguzi wa Baba, Mama na Mtoto jumla niTsh.300,000/=. Malipo yote hufanyika Benki.

5. Baada ya kukamilisha taratibu za malipo, sampuli za mpanguso wa kinywa(Buccal swab ) zitachukuliwa na watalaam katika maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi kulingana na Maombi ya Mteja.

6. Uchunguzi utafanyika na utakapokamilika majibu ya uchunguzi yatatolewa kwa taasisi iliyoandika barua ya maombi ya kufanyiwa uchunguzi na mteja husika atapata majibu yake kupitia taasisi hizo zilizoruhusiwa kisheria.

7. Majibu ya uchunguzi hutolewa kuanzia siku ya kumi na nne za kazi baada ya kuchukuliwa kwa sampuli.
 
Asante sana mkuu nimekusoma vema.
 
Back
Top Bottom