Naomba kujuzwa gharama za kufanya wiring

Wire 1.2mm? Wire 2.1mm? Siyo 1.5mm na 2.5mm? Kweli mambo yanabadilika haraka sana
 
Huu ni muandiko wako mkuu ama wa fundi mwenyewe? [emoji848]
Huo ni muandiko wa fundi, kaandika jina la kifaa, idadi na bei yake..
Mie nimepiga hesabu, pembeni kabisa.. Ukitizama vizuri uandishi wa namba zinatofautiana

Vipi kwani sheikh!?
 
roller moja la wire e.g. red bei gani boss? Switches na switch sockets umeweka? Bulb holders je? Earth wire na earth rod?

Roller nimeweka bei ni Tsh 30,000/= ,hivyo vingine havina issue maana bei yake ni ya kawaida sana,vyumba viwili vikorokoro hivyo haviwezi kuzidi elfu 30.
 
Huo ni muandiko wa fundi, kaandika jina la kifaa, idadi na bei yake..
Mie nimepiga hesabu, pembeni kabisa.. Ukitizama vizuri uandishi wa namba zinatofautiana

Vipi kwani sheikh!?
aah hapo penye vifaa vilivyoandikwa chini ya neno "maji" nilikua napata taabu kuvisoma vizuri. muandiko wa kifundi zaidi shekh wangu 😁

tunajifunza vitu kidogo ambavyo huenda siku moja vikatusaidia. 🤝
 
aah hapo penye vifaa vilivyoandikwa chini ya neno "maji" nilikua napata taabu kuvisoma vizuri. muandiko wa kifundi zaidi shekh wangu [emoji16]

tunajifunza vitu kidogo ambavyo huenda siku moja vikatusaidia. [emoji1666]
[emoji23]
 
Wire 1.2mm? Wire 2.1mm? Siyo 1.5mm na 2.5mm? Kweli mambo yanabadilika haraka sana
Sina hakika na hizo dimensions ila Siku hizi consumption kubwa ipo kwenye pasi labda wengi wetu tunatumia led ambazo ni very light kwenye current consuption.
 
Habari wakuu,

Naomba kujuzwa gharama ya kufanya wiring kwa room mbili tu, pamoja na vifaa vyote vinavyohitajika.
vifaa itakutoka si zaidi 120,000
ufundi siyo zaidi ya 100,000.

Angalizo:mwambie fundi akuandikie majina ya vifaa na kampuni,nenda katafute bei dukani mwenyewe.usikubali akupeleke yeye dukani,atapanga na muuzaji jinsi ya kukupiga kabla hamjaenda naye.Ila usinunue.siku ya kununua nenda naye. sababu vitu vingi vya umeme ni feki sana.Hasa kama uko Dar,kariakoo ndiyo sehemu wanapobambika sana

mambo mengine ni madoido tuu.
 
Nimepata muongozo!!!!!Je bei mlizozitaja hapo kwa tarehe hizi ni hizo hizo au zimebadilika?
 

Room 2 Main switch njia 4 ? Una socket na switch tu.

-Metal Box double - Kwa ajili ya socket kila chumba. -2 @1700=3,400

-Metal Box double - Nunua 1 hii ni kwaajili ya 2 gang light switch- moja itawasha chumba kimoja na nyengine itawasha nje.@1700=1,700

-Metal Box Single - Nunua 1 hii ni kwa ajili ya 1 Gang light switch itawasha chumba kimoja@1200=1,200

-Double switch sockets ( TRONIC) - Nunua 2@ 7500 = 14,000
-2 Gand light switch- Nunua 1@ 2500 = 2,500
-1 Gang light switch - Nunua 1@2000= 2,000
-Angle bulb holder - Nunua 3@1500=4,500

-Main switch chukua 3 ways ila hata 2 ways itafanya kazi vizuri kwa kuwa ni vyumba 2 tu ila nakushauri uchukue 3 ways@ 35,000 complete

-Earthrod 1@10000= 10,000
-2.5mm Earthwire 10m@900 = 9000

-Conduit pipe - 13@ 1400= 18,200
-2.5mm cable -20m@2200=44,000
-1.5mm cable - 24m@1500= 36,000
-4mm cable - 3m@3500= 10,500
-chukua misumari ya ceiling board kuishikilia conduit kama utaichimbia - 1/2kg @ 2500=1,250
-Elbow 15@300= 4,500
-Round box 3@500 = 1,500
-Junction box@1200 - muulize fundi wako
-Top cover @400 muulize fundi wako
-Bakora 1 @ 20,000 inategemea na fundi chuma
-Tanesco @27000 = 27,000
-Bulb 3 @2000= 6,000
-Mchoro na mambo ya mihuri kama 40,000 [emoji2][emoji846] hapa sijawahi fuatilia kuju a ndio utaratibu au watu wanapigwa

-Jumla ni Tshs - 292,250

-Tuongeze 15% ya dharura kama bei za material zimepanda and so on ..so inakuwa

Tshs 336,000

- Weka labour charge - 80,000- 100,000

Jumla 436,000
 
hizi size za 1.2mm na 2.1mm zinatumika wiring gani, mbona watu mnawalisha matango pori wadau,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…