Naomba kujuzwa gharama za material ya kutengeneza gril

Naomba kujuzwa gharama za material ya kutengeneza gril

Mh, mkuu kwa bei za sq. pipes sasa hivi naamini hizo bomba ni nyepesi mno.. 0.8mm tena nyeupe. Standard ya kawaida ni 1mm thickness, wenye uwezo wanatumia 1.2mm. Hiyo 100k hata materials tu ni kuungaunga.
0.8mm Una maana thickness ya bati iliotumika kutengeneza hizo square sio? It really don't matter to me.
Screenshot_20220515-202245.png
 
0.8mm Una maana thickness ya bati iliotumika kutengeneza hizo square sio? It really don't matter to me.
View attachment 2226045
Yeah, 0.8mm ni thickness ya bati ya bomba. Hii naona kama 1x1, looks cool. Wengi wetu hata hatujali hizo sijui thickness au nyeupe/nyeusi, ila wapo wanaojali sana.

Sasa imagine dirisha la 5x6ft linaingia bomba 5-6, bomba moja ya 1¼x1¼ ni 18,000.
 
Honestly hata mimi sikuwa na idea na hio thickness
 
Honestly hata mimi sikuwa na idea na hio thickness
Zipo hadi zenye 2mm, ndio unashangaa 1x1 inuzwa 28,000 wakati wewe unajua kawaida zinauzwa 12,000. Ukienda pale Tabata Sitta Steel wanauza rejects kwa bei nzuri sana.
 
Mlango kama huu unatakiwa kulipia bei gani? Kila kitu kwa fundi.
FB_IMG_1652112782881.jpg
 
Inafuatana na eneo,,2000 00mpaka 230000 yenye quality
Hawa watu wa grill kwenye milango ndio wanatupiga. Nikiangalia sqm za mlango hazizidi dirisha moja lakini bei mara mbili au hicho kipande cha bati gumu ni gharama sana?
 
Badala ya flat bar, tumia 12mm nondo, Square pipes au round pipes. Flat bar hazina uimara kabisa.

Frame 1¼×1¼ @16,000-18,000 inategemea wapi.
Partitioning 1x1 au ¾round pipe @13,000-15,000
Sticks no.10 5kg 22,000-25,000.
Cutting Disc @5,000
Grinding disc @5,000
Redoxide 4l @24,000
Brush 2½ @2,500
Bawaba @1,000
Stopper 12mm @2,500
Ufundi
Usafiri.

Usitumie flat bar, zina usalama mdogo.
Hapo inabidi atumie Bomba au Nondo.
 
Hawa watu wa grill kwenye milango ndio wanatupiga. Nikiangalia sqm za mlango hazizidi dirisha moja lakini bei mara mbili au hicho kipande cha bati gumu ni gharama sana?
Mkuu mlango unahitaji vitu vingi tofauti na dirisha,
Kuna bati, bawaba, chuma za fremu, chuma za ua lenyewe, ukipiga hesabu utaona kwa mfano mlango wa futi 8 urefu na futi 3 upana+;;;
Bomba za fremu ni 3@15000=45000/=
Bomba za ua ni 3@12000=36000/=
Bati jepesi nusu 45000/=
Bawaba 5000/=
Disck 6000/=
Stick 2kg =8000/=
Red oxide nusu lita 4000/=
Kwa hapo haiwezi kuwa sawa na dirisha bado ____________,,
Ufundi wa kazi ___
Komeo za kuchonga au za dukani ___
Usafiri wa kufuata hizo chuma???
 
Back
Top Bottom