Naomba kujuzwa haya kuhusu Jiji la Tanga

Wilhelm Johnny

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2016
Posts
1,368
Reaction score
1,325
Wakuu nilikuwa naomba kujuzwa frame Tanga Mjini bei gani pale Kati kati ya mji kabisa na changamoto za kibiashara zikoje na ule utamaduni wa kuona wazee ndio ufanye jambo bado upo.
 
- Fremu 50-200,000 kwa mwezi kutokana na vigezo vingi sana.

- Biashara challenge sana kutegemea na aina ya bishara.

- Hamna cha wazee wala nini.

- Biashara nzuri ya vyakula au mazao (mahindi, unga, mchele n.k)

- Nguo wale jamaa hawavai kabisa.
Shukrani mkuu hapo ni Tanga mjini center kabisa
 
- Fremu 50-200,000 kwa mwezi kutokana na vigezo vingi sana.

- Biashara challenge sana kutegemea na aina ya bishara.

- Hamna cha wazee wala nini.

- Biashara nzuri ya vyakula au mazao (mahindi, unga, mchele n.k)

- Nguo wale jamaa hawavai kabisa.
Hujui Tanga kabisa kijana wangu haswa kweny swala la nguo umechemka kama unabisha angalia bodaboda wa pale Tanga mjini then angalia wanawake wa Tanga .

Hakuna wanawake wanavaa kama wa Tanga Wana hata mtu ukute anakaa nyumba ya udongo anapikia kuni madera kama yote usiombe pawe na shughuli kama ya siku mbili nguo mpaka ya kuchambulia mchele .Mleta mada wanawake wa Tanga wanavaa haswa usidanganywe

Wanaume wanavaa sana na kupenda slope sema ijumaa wanapenda kanzu hata wakristo unakuta wanavaa kanzu.kingine nguo za special kwao dili mitumba Tangamano ipo kibao Tena mikali hawana ishu nayo na sasa vijana wengi hawataki kazi kupindisha midomo huko Instagram na Facebook kwa nguo za kuazima maana hawana hela za ila wanapenda kuvaa sijawai kuona .....Angalia bodaboda wa Tanga utaona jinsi wanavyopenda kuvaa special vunjabei alishtuka mchongo kashaweka duka pale Yale maronya yake yananunuliwa sana .

Kingine Tanga hamna watu wengi pale town kumepoa Sana wengi wamehama wanakimbilia kange na njia ya mwahako

Kuhusu nafaka umepatia ukiangalia ndo zinawatajirisha wasambaa rejea mashine za unga pale barabara 15.
 
Mitaa iliyochangamka kibiashar ni ipi ni ipi yani watu wa kutoka pembezoni mwa mji wanaenda fanya manunuzi kwa wingi kama dar kariakoo Dodoma barabara ya sita mpaka ya kumi
 
Ndiyo hapo sawa umemuweka sawa eid tanga week mbili.
 
Mitaa iliyochangamka kibiashar ni ipi ni ipi yani watu wa kutoka pembezoni mwa mji wanaenda fanya manunuzi kwa wingi kama dar kariakoo Dodoma barabara ya sita mpaka ya kumi
Barabara ya 13 kwa ajili ya nguo ,na 15 kwa biashara za nafaka, mgandini pale kwa matunda na mbogamboga yaani sokoni ,mitumba Tangamano hapo wateja kibao jumamosi na jumanne na alhamisi kipindi natoka mwaka 2013 ilikuwa ivyo so sijui kwa sasa
 
Mimi nataka niende kwa ajili ya vifaa vya simu
 
Mimi nataka niende kwa ajili ya vifaa vya simu
Barabara ya 13 na stendi ya zamani pale pako poaw sana nasikia kuna stendi mpya huko kange sijawai kufika nimeondoka kitambo sijajua biashara zipoje ? huko kange.
 
Nilichokipenda tanga..ni mji umepangika sana..pia migawani chakula kitamu sana..hakika tanga kwa mapishi wako vizuri.

#MaendeleoHayanaChama
 
- Fremu 50-200,000 kwa mwezi kutokana na vigezo vingi sana.

- Biashara challenge sana kutegemea na aina ya bishara.

- Hamna cha wazee wala nini.

- Biashara nzuri ya vyakula au mazao (mahindi, unga, mchele n.k)

- Nguo wale jamaa hawavai kabisa.
Hahahaha Tanga Wanagonga Kanzu Tuu[emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…