Naomba kujuzwa, ikiwa kuna msamaha wa kodi (customs)kwa mfanyakazi wa serekali anayenunua /kuagiza gari nje ya nchi

Mtananaz

Member
Joined
Jun 4, 2023
Posts
7
Reaction score
10
Wadau nifahamisheni ikiwa kuna punguzo ama msamaha wa kodi kwa mfanyakazi wa Serekali anayeingiza gari nchini ikiwa gari limetengenezwa ndani ya miaka 10
 
Wadau nifahamisheni ikiwa kuna punguzo ama msamaha wa kodi kwa mfanyakazi wa Serekali anayeingiza gari nchini ikiwa gari limetengenezwa ndani ya miaka 10
Kama wewe ni mtumishi wa Umma, ndiyo kuna kusamehewa kwa Ushuru wa Forodha. Ila utalipa VAT pamoja na Excise duty.

Gari linapaswa kuwa na umri chini ya miaka kumi tangu kutengenezwa kwake. Pia, lisiwe gari la biashara (kubeba abiria). Wanaangalia na CC.

Unaweza kutembelea TRA kwa maelezo zaidi.
 

Cha kuongeza,

Watumishi waumma wapo baadhi hawapati hadi wawe na cheo cha afisa, kwa maana madereva, secretaries etc hawapati ila nadhani kwa walimu ni wote.
Msamahana ni wa Import duty na Excise duty due to CC ila ikiwa gari ina miaka 8,9 au 10 utalipa na Excise duty due to Age. Ikiwa na miaka 7 hadi 0 hulipi uchakavu...na gari isizidi CC 3000 kwa maana hizo ndio ukomo wa msamaha wa kodi.

Kwa utaratibu zaidi unaweza ukaniPM ili kuhadithie mchakato mzima hadi upate gari yako na uwahi kuitoa kabla haijaanza kupata storage.
 
Aaah shukran mkuu, natamani kujua ni wakati gani unapaswa kuomba kabla au ukishalinunua likiwa majini

Aaah shukran mkuu, natamani kujua ni wakati gani unapaswa kuomba kabla au ukishalinunua likiwa majini linakuja?
Likiwa majini linakuja,kuna document umetumiwa toka japan ndo hizo zipeleke wanazihitaji ili kuconferm mwaka wa gari,cc na kama sio la kibiashara na mambo mengine.kwa uhakika zaid visit TRA watakupa taarifa kamili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…