Naomba kujuzwa kati ya Toyota Spacio v/s Toyota Wish

SAMAP

Member
Joined
Nov 15, 2018
Posts
45
Reaction score
17
Kati ya Toyota Spacio na Toyota Wish ipi ni imara na inafaa kwenye mazingira yetu ya barabara mchanganyiko (tembea kidogo kwenye rami na kidogo kwenye vumbi)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nilichoona kwa shemeji yangu na jirani yetu chukua spacio.

Wish body yake inaharibika fasta ikiwa itatumika kwenye vumbi na makorongo.
 
Kiufupi gari lolote ni utunzaji na nidhamu ya service zenye ubora....kuna mtu unaweza kumpa land rover 109 akaichakaza ikaisha akamuacha mtu na passo yake anadunda

Sent using Jamii Forums mobile app
Ninakubaliana nawe 100%. Kila mtu aliyekiona chombo changu 2014, leo hii akikiona anashangaa kuwa mbona kipo vilevile!
 
Kiufupi gari lolote ni utunzaji na nidhamu ya service zenye ubora....kuna mtu unaweza kumpa land rover 109 akaichakaza ikaisha akamuacha mtu na passo yake anadunda

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni kweli kabisa. Hizo gari zote materials ni more or less the same. Kusema body la Wish ni laini kuliko Spacio wala sidhani kama ni kweli. Sema Wish ni ndefu tu (long wheelbase) sasa kwenye makorongo inahitaji umakini zaidi. Watu wengi wanaoziendesha kwa kweli wana zi abuse. Vile zinabeba watu 7, jamaa wanafikiri ni Land Cruiser. Wanataka kwenda nazo kwa bibi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…