Naomba kujuzwa kuhusu gari aina ya Toyota Verso

Mkuu kama ndiyo unataka kuinunua hiyo gari jitafakari mara mbili.

Kwa haraka haraka hiyo ndinga isharudiwa rangi hapo ilipo,sasa ni jukumu lako kujua sababu iliyofanya rangi irudiwe.

Pia kwa muonekano inaonekana injini yake inaangukia kwenye cc 1490
 
Mie naomba kuelimishwa ni kwa nini gari ikipigwa rangi linakuwa kosa?
Sio kosa mkuu,ila inapoteza ile nuru original iliyokuja nayo hivyo inapoteza mvuto kipindi unapotaka kufanya biashara.
 
Imepigwa rangi ya stoo
 
Vigari vidogo dogo hivi huwa sina mzuka navyo kabisa.

Gari la mwanaume ni Crown,Premier au Harrier
Mkuu sijui unaishi wapi ila haya uliyoyataja ni mahsusi kwa wavulana tu na sio wanaume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…