Naomba kujuzwa kuhusu hii gari inayoitwa Honda Crossroad

Naomba kujuzwa kuhusu hii gari inayoitwa Honda Crossroad

Holly Star

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Posts
4,327
Reaction score
8,142
Waheshimiwa saaaana, heshima kwenu.

Niende kwenye mada moja kwa moja, nimekuwa mtumiaji wa passo kwa miaka kama 5 hivi, nimeendesha passo 2 hadi sasa
Baada ya corona kuingia nliacha kabisa kusafiri na public transport nikawa naendesha passo yangu dar mwanza dar, ninaposafiri mkoani kikazi. Sasa nahisi kuichoka japo haijawahiniangusha kabisa. Safari zangu huenda bila shida tena nonstop.

Nimerecomend hii gari kwa marafiki zanfu 3 na wameagiza wanaidrive nimeona kama ni gari nzuri na ni fuel economy kwa cc 1790. Na mm huwa napendelea kusanya abiria njiani hivo jikiwa na safari nitaenda bila matatizo sababu ni 7 seaters.

Nimekuja kwenu kuomba kujuzwa ubora wa hii gari, kwa mwonekano wake naipenda kwa 90%. Ubora wa gari sijaujua vizuri.

images%20(12).jpg

Nunua tu Mkuu, nilishaifatilia mtandaoni iko vizur Mana ni min SUV rough road inapita vizur , consupt.ni 1ltr per 13 km, upande wa spear kwa dar huwez hangaika labda kwa wale wa mikoan ndo shida kidogo.
 
Lakini mleta mada, ni kama unatuchanganya.

Umetueleza sababu ya kukwepa usafiri wa jumuiya, hapo hapo unafanya ambacho hua unakwepa kwenye usafiri wa jumuiya.
1 anapakia, yeye ndio mwenye mamlaka
2 anapakiwa, hana mamlaka

Hapo ndio alipolenga.
 
Kuna za kawaida na Hybrid. Kama anapenda mbio na ubabe road Achukue Honda Accord atakuwa wanapambana na kina Crown, BMW na Benz.
Kwa kuepuka kuwaza wese, naona hybrid ni teknolojia kimbilio kwa sisi huku afrika, kabla ya kuhamia kwenye umeme full 2050.
 
Kwa kuepuka kuwaza wese, naona hybrid ni teknolojia kimbilio kwa sisi huku afrika, kabla ya kuhamia kwenye umeme full 2050.
Gari ya umeme haina Raha, mkuu achana na utamu wa internal combustion engine iwe ni diesel au petrol.

Nyie hamieni kwenye hybrid au umeme ila gari ya mafuta bado Sana itakuwepo. Baadhi ya nchi wanatengeneza biodiesel ambayo haichafui mazingira Kama diesel ya kuchimbwa.
 
Unaposema ndoa ya kikristo una maanisha nn! Kwamba haiuziki tena?kwani mtu akinunua gari ni lazima aje aliuze!!!???

Ndio zinavyoitwa mkuu,yes sio lazima auze ila akitaka pia kuuza haliuziki na ndio maana wakaita "NDOA YA KIKRISTO".
 
Ndio zinavyoitwa mkuu,yes sio lazima auze ila akitaka pia kuuza haliuziki na ndio maana wakaita "NDOA YA KIKRISTO".
Honda ni moja ya magari imara sana. Vipuli vyake vingi bado ni genuine na hapo ndiyo huipa gari thamani inayostahili. Performance side, ni gari zenye performance nzuri sana. Unaponunua gari leo kigezo cha kuliiuza baadae usikiweke, gari huuzwa likiwa kwenye hali nzuri na bei muafaka. Nunua kutokana na performance na pia mahitaji yako.
 
Ahsante ndugu..gari ni sawa na vifaa/Mashine nyingine unazoweza kununua,na sijui ni kwa nini watu huwaza jinsi ya kuuza gari lake kabla hajalinunua na wala sio kwa vifaa vingine kama TV,Radio,Sofa seats NK
 
Back
Top Bottom