Naomba kujuzwa kuhusu hili la Martrial Arts

mzee wa kasumba

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
1,440
Reaction score
2,952
Bwana we!

Kuna hizi sanaa za mapigano aina tofauti tofauti.

Maswali yangu ni haya hapa yafuatayo:

1. Hivi kuna ambazo ni hatari zaidi kuliko nyingine ama inategemea na umahiri wa mtu?

2. Ile mikanda inayotolewaga na kuvaliwa viunoni, utaratibu wake ni mmoja ama kila fani ina utoaji wake wa mikanda?

3. Kwa mtu mzima (miaka 40 - 60) ambaye anataka kuokota mbili tatu. Ni upi mchezo mzuri kwake?

Wajuzi naomba ujuzi

#Kung fu
#Boxer
#Kick boxer
#Taekwondo
#Kombat karate
#Guju ryu
#Krav maga
#Muay thai
#Jiu - jitsu (brazilian)
#Judo
#Na kadhalika
 
Mkuu mi binafsi ni member wa Tae kwon do na jit kwon do umahili wako katika kutumia kile ulichofunzwa ndio kinakufanya uwe bora zaidi pia incase kuna teknic hizi huwa zipi nyingi mno mkuu, we pia ukiwa na umri wa miaka hiyo unaweza fuzwa..
White belt
Yellow belt
Green belt
Blue Belt

Na hiyo miwili iliyobaki ya high level...
 
Ooooh saw saw mkuu... Ila mimi binafsi umri wangu ni 31. Si umri nilioutaja hapo juu.

Sema qumer zimetumaliza kwishney[emoji3][emoji3]
 
Inategemeana na umahiri wa mtu. Na pia unaitumia wapi.
 
Dah! Hii michezo siwezi kuisahau! Nakumbuka wakati nasoma Kidato cha Pili nilijiunga na Guju ryu baada ya kutimiza kama wiki moja hivi nilitamani atokee Mtu nipigane nae! Sikuhiyo Mtaani nilikuta Madogo watatu kuna kademu cha Mtaani wanakizongazonga si nikajifanya Steringi wa kihindi kutuliza shoo! Kudadeki Walinidunda mpaka Akatokea Mzee mmoja Jirani kuja kuniombea! Mbona maji niliita mma 😂😂😂
 
Kwa umri wako ungemrudia muumba wako kuliko hiyo michezo

Kwanini usicheze ata kwaya za kanisani/ kaswidah
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wing Chun ndio nzuri.

Kama umri umekutupa mkono bora ununue mbundu(bastola)/uanze kusali sana/au ununue uchawi Kwa ajili ya kujilinda, Maisha ni yale yale.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wing Chun ndio nzuri.

Kama umri umekutupa mkono bora ununue mbundu(bastola)/uanze kusali sana/au ununue uchawi Kwa ajili ya kujilinda, Maisha ni yale yale.
[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Niliicheza hii michezo kuanzia miaka ya 1999,na kaka zangu wote wameicheza sana ,Hakika ni mizuri,inahitaji mda na moyo wa kujituma.

Ni hatari sana kama huna kazi nyingine ya kukuingizia kipato,kuna baadhi waliishia kuwa majambazi,na wengine ni ma master hadi leo hii.
Ina chukua mda mtu kuiva hasa na inatakiwa kichwa cha kushika mambo.
 
Kwa umri wako ungemrudia muumba wako kuliko hiyo michezo

Kwanini usicheze ata kwaya za kanisani/ kaswidah
[emoji3][emoji3][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] duh! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Dah!
 
Martial arts hutegemea na muhusika ana ubora gani katika mapambano.
Mfano hiyo krav maga huwa ni self defense martial arts ambayo inatumiwa sana na special forces za Israel haina mfumo wa mikanda wala haina kata.

Pia Muay Boran ni martial arts ambayo inatumiwa sana Thailand ni martial art isiyo na belt pia. Na ilitumiwa zaidi na askari katika vita ni hatari kubwa sana kutumia techniques zake ndiyo maana ilipunguzwa baadhi ya techniques na wakapata Muay Thai.

Martial nyingine nyingi hutumika katika mashindano ila pia hutumika majeshini kwa kuongezewa baadhi ya vitu ambavyo ni deadly.

Kuhusu umri kuna martial arts zinakuhitaji sana uanze na umri kati ili kufanya viungo visipate madhara pia katika moyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…