Salamu wana jukwaa kwa ujumla...
Napenda kutanguliza shukurani za dhati, kwa wote wanaotupa elimu kuhusiana na sekta ya kilimo kwa ujumla na faida zake, hasa changamoto na faida za mazao ya biashara.
Nimeshawishika sana na zao la Tumbaku kwa ujumla, na mwaka huu mwezi wa 12 napenda kuanza kilimo chake, ningependa kwa wale wazoefu wa zao hili waweze kutupa changamoto na faida zake za ujumla.
Asanteni.
Moja ya mazao biashara yakipumbavu kwa mkulima na very poor earnings Sanasana kuharibu misitu na uoto wa akili.
1. Unashughulika 12month
2. Unapambana na kazi ngumu 12month
3. Unatumia gharama kubwa maandalizi, madawa, nk
4. Unavuna kwa shida
5. Unagrade vizuri kabisa kwenye madaraja stahiki
6. Unafunga kwenye malobota
7. Unabeba kupeleka godown/warehouse for sale
8. Anakuja mnunuzi ana- value/ anakupa lowest grades ever kwenye tumbaku yako
9. Unauza kwa hasara, sababu umehujumiwa kwenye grades
10. Ukipata Malipo fanya mgawanyo wa total received bila kuondoa running cost gawanya kwa participants ...... kwakila kiwango kwa mtu mmoja gawanya kwa mwizi 12 ....
A) Average earnings before deduction of other costs kwa mwezi it will be not more than tsh 500,000.
B) Average cost per person after all other deductions kwa mwezi haitazidi 100,000 yaani total profit per year haitazid tsh 1,000,000 per head per year.
In summary usijishughulishe na biashara kichaa ya kilimo cha tumbaku utakufa maskini na utajutia muda wako.
Bora ufanye yafuatayo
1. Ufugaji..... kuku, ng'ombe wa maziwa, nguruwe nk
2. Kilimo cha matunda Hususani machungwa, machenza nk
3. Kilimo cha pamba, kahawa, chai nk
Tumbaku sio kabisaaaaa