Naomba kujuzwa kuhusu kilimo cha tumbaku Tanzania

Naomba kujuzwa kuhusu kilimo cha tumbaku Tanzania

Mkuu achana na kilimo hicho kitakupotezea mda na fedhe nyingi nimebahatika kupita kwa wakulima mbali mbali wa Tumbaku mkoani Mbeya kuanzia Chunya ,Lupa, Isangawana, Bitimanyanga, Kambi katoto na Upande wa Tabora na Singida aisee hali ni tete Mabalo ya Tumbaku hayana bei na yamerundikana Godown hakuna wa kununua mbaya zaidi unakuta Tumbaku hadi ya mwaka p bado iko Ghalani sasa sijui hii utakayo I zalishwa itaende wapi?

Kama unataka kutoboa kupitia Kilimo lima mazao yafuatayo

1 Alizeti hakikisha unatumia kilimo cha kisasa na baada ya mavuno nenda kiwandani na uuze mafuta mwenyew usiuze Alizeti

2 ufuta

3 Dengu

4 Choroko

5 Maharage

6 Mahindi mabichi ya kumwagilia
Asante sana ndugu kwa ushauri wako mzuri ntaufanyia kazi
 
Poleni na mihangaiko pamoja na mapambano ya kujikiga na Covid-19. Kuna watu nikiwa kwenye daladala leo nimewafuatilia sana mazungumzo yao juu ya kilimo hiki cha tumbaku na hivyo nami nikavutika kuingia kwenye kilimo hiki.

Naombeni elimu zaidi juu ya kilimo cha tumbaku hasa
Asanteni.
 
Poleni na mihangaiko pamoja na mapambano ya kujikiga na Covid-19.
Kuna watu nikiwa kwenye daladala leo nimewafuatilia sana mazungumzo yao juu ya kilimo hiki cha tumbaku na hivyo nami nikavutika kuingia kwenye kilimo hiki.

Naombeni elimu zaidi juu ya kilimo cha tumbaku hasa
Asanteni.
Aisee

Utaiuzia wapi mkuu ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumbaku lilikuwa zao zuri sana la kupigia hela kabla hii serikali ya tano haijaharibu mambo.

Leo hii Bashe anatuambia tuuze tumbaku yetu kwa gulio kama chupi za mtumba ???

Dah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee

Utaiuzia wapi mkuu ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna makampuni yapo hununua kila mwaka. Kilo moja huuzwa hadi zaidi ya elfu 6 ila wakulima wengi huzalisha tumbaku ya kufaa kuuzwa kwa wastan wa dola 1.5 had dola mbili.

Pembejeo hukopeshwa kwa wakulima na pia kiasi cha kilo kuweza kuzalishwa hukadiriwa na serikali.
 
Moja ya mazao biashara yakipumbavu kwa mkulima na very poor earnings Sanasana kuharibu misitu na uoto wa akili.

1. Unashughulika 12month

2. Unapambana na kazi ngumu 12month

3. Unatumia gharama kubwa maandalizi, madawa, nk

4. Unavuna kwa shida

5. Unagrade vizuri kabisa kwenye madaraja stahiki

6. Unafunga kwenye malobota

7. Unabeba kupeleka godown/warehouse for sale

8. Anakuja mnunuzi ana- value/ anakupa lowest grades ever kwenye tumbaku yako

9. Unauza kwa hasara, sababu umehujumiwa kwenye grades

10. Ukipata Malipo fanya mgawanyo wa total received bila kuondoa running cost gawanya kwa participants ...... kwakila kiwango kwa mtu mmoja gawanya kwa mwizi 12 ....

A) Average earnings before deduction of other costs kwa mwezi it will be not more than tsh 500,000.

B) Average cost per person after all other deductions kwa mwezi haitazidi 100,000 yaani total profit per year haitazid tsh 1,000,000 per head per year.

In summary usijishughulishe na biashara kichaa ya kilimo cha tumbaku utakufa maskini na utajutia muda wako.

Bora ufanye yafuatayo
1. Ufugaji..... kuku, ng'ombe wa maziwa, nguruwe nk

2. Kilimo cha matunda Hususani machungwa, machenza nk

3. Kilimo cha pamba, kahawa, chai nk

Tumbaku sio kabisaaaaa
Acha kupotosha wenzio mkuu, Acha wajionee mbona pesa ipo labda kipindi cha magu ndo soko liliyumba kidogo
 
Mkuu achana na kilimo hicho kitakupotezea mda na fedhe nyingi nimebahatika kupita kwa wakulima mbali mbali wa Tumbaku mkoani Mbeya kuanzia Chunya ,Lupa, Isangawana, Bitimanyanga, Kambi katoto na Upande wa Tabora na Singida aisee hali ni tete Mabalo ya Tumbaku hayana bei na yamerundikana Godown hakuna wa kununua mbaya zaidi unakuta Tumbaku hadi ya mwaka p bado iko Ghalani sasa sijui hii utakayo I zalishwa itaende wapi?

Kama unataka kutoboa kupitia Kilimo lima mazao yafuatayo

1 Alizeti hakikisha unatumia kilimo cha kisasa na baada ya mavuno nenda kiwandani na uuze mafuta mwenyew usiuze Alizeti

2 ufuta

3 Dengu

4 Choroko

5 Maharage

6 Mahindi mabichi ya kumwagilia
Mkuu ulicho andika hapa ni porojo za vijiweni

kwa ufahamu wangu tumbaku hununuliwa kupitia vyama vya msingi na kabla ya yote chama huakikisha wana kampuni ya kununua zao lao kabla ya wakulima kuanza kulima

Tumbaku inapelekwa vipi? Godauni na haina mnunuzi Hadi ikae na kumaliza mwaka huko
 
Acha kupotosha wenzio mkuu, Acha wajionee mbona pesa ipo labda kipindi cha magu ndo soko liliyumba kidogo
Mkuu tumbaku Ina hela mnooo

Maggu aliwakopa fedha flani Hadi jamaa wakaacha toa malipo ya bonusi kwa wakulima

Mama samiah nae alikuja na tozo (kodi) kwenye tumbaku ila baada ya malalamiko ilitolewa

Sema mziki upo mwaka kesho nimeona pembejeo imepanda mara 2 ya mwaka huu maana mwaka huu n.p.k ya tumbaku ni usd 48.77 ila mwakani iko 70.77, can iko 26.03 ila mwakani ni 59.99

Kikao cha kupanga bei ya tumbaku nahisi kinakaaa mwezi ujao kama hawata pandisha bei mara 2 pia kilimo kinaenda kuwa kigumu mnooo

Japo nilisikia wanataka weka ruzuku kama wasipo Fanya hivyo mkulima anaenda umia balaaa
 
Back
Top Bottom