Naomba kujuzwa kuhusu kilimo cha tumbaku Tanzania

Asante sana ndugu kwa ushauri wako mzuri ntaufanyia kazi
 
Poleni na mihangaiko pamoja na mapambano ya kujikiga na Covid-19. Kuna watu nikiwa kwenye daladala leo nimewafuatilia sana mazungumzo yao juu ya kilimo hiki cha tumbaku na hivyo nami nikavutika kuingia kwenye kilimo hiki.

Naombeni elimu zaidi juu ya kilimo cha tumbaku hasa
Asanteni.
 
Aisee

Utaiuzia wapi mkuu ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumbaku lilikuwa zao zuri sana la kupigia hela kabla hii serikali ya tano haijaharibu mambo.

Leo hii Bashe anatuambia tuuze tumbaku yetu kwa gulio kama chupi za mtumba ???

Dah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee

Utaiuzia wapi mkuu ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna makampuni yapo hununua kila mwaka. Kilo moja huuzwa hadi zaidi ya elfu 6 ila wakulima wengi huzalisha tumbaku ya kufaa kuuzwa kwa wastan wa dola 1.5 had dola mbili.

Pembejeo hukopeshwa kwa wakulima na pia kiasi cha kilo kuweza kuzalishwa hukadiriwa na serikali.
 
Acha kupotosha wenzio mkuu, Acha wajionee mbona pesa ipo labda kipindi cha magu ndo soko liliyumba kidogo
 
Mkuu ulicho andika hapa ni porojo za vijiweni

kwa ufahamu wangu tumbaku hununuliwa kupitia vyama vya msingi na kabla ya yote chama huakikisha wana kampuni ya kununua zao lao kabla ya wakulima kuanza kulima

Tumbaku inapelekwa vipi? Godauni na haina mnunuzi Hadi ikae na kumaliza mwaka huko
 
Acha kupotosha wenzio mkuu, Acha wajionee mbona pesa ipo labda kipindi cha magu ndo soko liliyumba kidogo
Mkuu tumbaku Ina hela mnooo

Maggu aliwakopa fedha flani Hadi jamaa wakaacha toa malipo ya bonusi kwa wakulima

Mama samiah nae alikuja na tozo (kodi) kwenye tumbaku ila baada ya malalamiko ilitolewa

Sema mziki upo mwaka kesho nimeona pembejeo imepanda mara 2 ya mwaka huu maana mwaka huu n.p.k ya tumbaku ni usd 48.77 ila mwakani iko 70.77, can iko 26.03 ila mwakani ni 59.99

Kikao cha kupanga bei ya tumbaku nahisi kinakaaa mwezi ujao kama hawata pandisha bei mara 2 pia kilimo kinaenda kuwa kigumu mnooo

Japo nilisikia wanataka weka ruzuku kama wasipo Fanya hivyo mkulima anaenda umia balaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…