Wakuu habari za muda huu.
Nakuja mbele yenu na mambo kadhaa ambayo naomba mwenye kujua chochote juu yake anijuze.
Hivi, wachoraji wa picha za tingatinga zile rangi wanazotumia ni rangi za aina gani ( zinaitwaje ). Je kitambaa ambacho hutumika kuchorwa picha ni kitambaa tu chochote au kuna aina za vitambaa vyake vya shughuli hii?. Na je nikihitaji frem ili picha niiweke ndani ya frem wapi nitapata frem nzuri.
Na je hizi rangi, kitambaa, wapi ntavipata vitu hivi? Na je bei ikoje???. Mimi naishi Dar.
Naomba kuwasilisha ndugu zangu.
Wakuu habari za muda huu.
Nakuja mbele yenu na mambo kadhaa ambayo naomba mwenye kujua chochote juu yake anijuze.
Hivi, wachoraji wa picha za tingatinga zile rangi wanazotumia ni rangi za aina gani ( zinaitwaje ). Je kitambaa ambacho hutumika kuchorwa picha ni kitambaa tu chochote au kuna aina za vitambaa vyake vya shughuli hii?. Na je nikihitaji frem ili picha niiweke ndani ya frem wapi nitapata frem nzuri.
Na je hizi rangi, kitambaa, wapi ntavipata vitu hivi?. Na je bei ikoje??. Mimi naishi Dar.
Naomba kuwasilisha ndugu zangu.
Shukrani sana mkuu na ubarikiwe.Mkuu Mimi ni mdau, ngoja nikujibu maswali yako na kama una swali lolote kuhusu Painting unaweza kuuliza.
Tingatinga artworks zinachorwa kwa kutumia Vitambaa vyeupe, vigumu (Japo wapo hutumia vyepesi kwa kupoza gharama).
Kwa Tanzania artist wengi hutumia kitambaa kinaitwa Marekani, pia hutumika kama Sanda.
Kitambaa huwambwa kwenye frame ya mbao (kuna aina mbili za frame kwenye Painting)
1.Canvas frame; hii ndo hutumika kuchorea.
2.frame ya kioo; hutumika kuweka picha iliyochorwa tayari kwa matumizi.
Kwa wenzetu nje ya Tanzania hutumia Kitambaa kigumu zaidi.
Rangi zinazotumiwa kwa ajiri ya Background kwa Tanzania tunatumia Silk ya maji, coz ndo high quality water paint.
Rangi tunazotumia kuchorea kuna za Maji na Mafuta....
Kwa maji tunatumia Acrylic za kopo, pia zipo za tube.
Kwa mafuta hutumia za Kopo pia zipo za tube...
Japo rangi za mafuta sio mradi za mafuta tu, zipo special kwa ajiri ya kuchorea, ambazo sio transparent.
Frame kama ni za Kioo unaweza kwenda Morogoro store kama unatokea CCBRT (Ila ni bei mbaya)
Kama ni kwa ajiri ya Kuchorea, unaweza kumpa kazi fundi akakutengenezea (kuna vipimo ambavyo huwa uniform Worldwide, japo hutofautiana kidogo)
Nadhani nimejaribu kukujibu.
Rangi za Silk zinauzwa kwenye Hardware.Shukrani sana mkuu na ubarikiwe.
Na kwa Dar es salaam wapi ntapata hizi rangi za silk na bei ikoje.