Naomba kujuzwa mambo kadhaa kuhusu uchoraji wa picha kama tingatinga

Tanki

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
538
Reaction score
246
Wakuu habari za muda huu.

Nakuja mbele yenu na mambo kadhaa ambayo naomba mwenye kujua chochote juu yake anijuze.
Hivi, wachoraji wa picha za tingatinga zile rangi wanazotumia ni rangi za aina gani ( zinaitwaje ). Je kitambaa ambacho hutumika kuchorwa picha ni kitambaa tu chochote au kuna aina za vitambaa vyake vya shughuli hii?. Na je nikihitaji frem ili picha niiweke ndani ya frem wapi nitapata frem nzuri.

Na je hizi rangi, kitambaa, wapi ntavipata vitu hivi?. Mimi naishi Dar.

Naomba kuwasilisha ndugu zangu.
 
Wakuu habari za muda huu.

Nakuja mbele yenu na mambo kadhaa ambayo naomba mwenye kujua chochote juu yake anijuze.
Hivi, wachoraji wa picha za tingatinga zile rangi wanazotumia ni rangi za aina gani ( zinaitwaje ). Je kitambaa ambacho hutumika kuchorwa picha ni kitambaa tu chochote au kuna aina za vitambaa vyake vya shughuli hii?. Na je nikihitaji frem ili picha niiweke ndani ya frem wapi nitapata frem nzuri.

Na je hizi rangi, kitambaa, wapi ntavipata vitu hivi? Na je bei ikoje???. Mimi naishi Dar.

Naomba kuwasilisha ndugu zangu.
 
Wakuu habari za muda huu.

Nakuja mbele yenu na mambo kadhaa ambayo naomba mwenye kujua chochote juu yake anijuze.
Hivi, wachoraji wa picha za tingatinga zile rangi wanazotumia ni rangi za aina gani ( zinaitwaje ). Je kitambaa ambacho hutumika kuchorwa picha ni kitambaa tu chochote au kuna aina za vitambaa vyake vya shughuli hii?. Na je nikihitaji frem ili picha niiweke ndani ya frem wapi nitapata frem nzuri.

Na je hizi rangi, kitambaa, wapi ntavipata vitu hivi?. Na je bei ikoje??. Mimi naishi Dar.

Naomba kuwasilisha ndugu zangu.
 
Kwa msaada tembelea instagram andika neno, WORLD OF PENSILS, angalia vifaa wanavyotumia kuchora.
 
Kwema Mkuu. Picha mfano wa Tingatinga hutumia vitambaa vya kawaida vizito ambavyo havipitishi rangi kwa urahisi (tetron) mfano wa vitambaa vinavyochorewa matangazo.

Rangi zinazotumika ni rangi za maji (water colours).
Rangi za maji zipo za aina nyingi kuna Silk , watherguard n.k. Pia unaweza tumia rangi za mafuta (oil painting) japo wengi hawatumii kwasasa.

Vitambaa vinapatikana kwa mafundi nguo, wanauza mita 1 2000/=.
Flame unaweza chongesha mwenyewe au kwa fundi Mbao au Kwenye Stationery.
Rangi hzo sijui kwa Dar mahala wanauza ila Mwanza kuna jamaa anaitwa Pongoro maeneo ya Natta.
Bei ya rangi inategemea na ujazo na aina ya rangi. Inaanzia elfu 5 kwa nusu lita.
 
Mkuu Mimi ni mdau, ngoja nikujibu maswali yako na kama una swali lolote kuhusu Painting unaweza kuuliza.

Tingatinga artworks zinachorwa kwa kutumia Vitambaa vyeupe, vigumu (Japo wapo hutumia vyepesi kwa kupoza gharama).

Kwa Tanzania artist wengi hutumia kitambaa kinaitwa Marekani, pia hutumika kama Sanda.

Kitambaa huwambwa kwenye frame ya mbao (kuna aina mbili za frame kwenye Painting)
1.Canvas frame; hii ndo hutumika kuchorea.
2.frame ya kioo; hutumika kuweka picha iliyochorwa tayari kwa matumizi.

Kwa wenzetu nje ya Tanzania hutumia Kitambaa kigumu zaidi.

Rangi zinazotumiwa kwa ajiri ya Background kwa Tanzania tunatumia Silk ya maji, coz ndo high quality water paint.

Rangi tunazotumia kuchorea kuna za Maji na Mafuta....
Kwa maji tunatumia Acrylic za kopo, pia zipo za tube.
Kwa mafuta hutumia za Kopo pia zipo za tube...
Japo rangi za mafuta sio mradi za mafuta tu, zipo special kwa ajiri ya kuchorea, ambazo sio transparent.

Frame kama ni za Kioo unaweza kwenda Morogoro store kama unatokea CCBRT (Ila ni bei mbaya)
Kama ni kwa ajiri ya Kuchorea, unaweza kumpa kazi fundi akakutengenezea (kuna vipimo ambavyo huwa uniform Worldwide, japo hutofautiana kidogo)

Nadhani nimejaribu kukujibu.
 
Shukrani sana mkuu na ubarikiwe.

Na kwa Dar es salaam wapi ntapata hizi rangi za silk na bei ikoje.
 
Rangi za Silk zinauzwa kwenye Hardware.
20 litres - 120,000
10 litres - 70,000
4 litres - 35,000 - 40,000
 
Back
Top Bottom