Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante sana kwa ushauri nitaufanyia kazi!Kuhusu unyevu nimeanza kuianika!Hiyo mycotoxin nitaitafuta.Swali langu ni hivi hiyo dawa haina "effect" yoyote kwa kuku?Maana lengo langu nikuja kuiuza hiyo pumba ikiwa imechanganywa na virutubisho vingine kwa ajili ya kuku,sungura n.k!Kwa nini ninakusanya hii pumba,ni kwa sababu eneo nililopo wafugaji wameongezeka halafu kuna wakati pumba inaadimika kabisa!Hufikia sh.6000 kwa debe ilhali kwa sasa ni sh.3000Manunuzi ya pumba yaendane na uhitaji kwa maana pumba haswa kutokana na kiasi cha unyevu inayokua nayo inawahi kuvunda (kutengeneza fangasi) na kuzalisha sumu kuvu kwa kitaalamu zinaitwa Mycotoxins.
Ufanyaje?
1. Hakikisha pumba inaanikwa kwenye turubai nje kwa ajili ya kupigwa na upepo na jua ili kupunguza kiasi cha unyevu. Unyevu mwingi husababisha pumba kuvunda haraka. Unyevu ukipungua pumba itakaa kwa muda mrefu
2. Usinunue pumba nyingi sana kuliko kiasi cha mahitaji ya kuku. Jitahidi kufanya makadirio ya manunuzi yako ukiangalia uhitaji. Pumba nyingi sana ni ngumu kuisimamia bila kutengeneza sumu kuvu
3. Kuna dawa za kuchanganyia kwenye pumba kupunguza sumu kuvu (mycotoxins) ambazo zinaitwa Mycotoxin binder. Unachanganya na pumba na zinashibiti kwa kiasi kikubwa sumu hiyo ya fangasi. Nenda duka la madawa ya mifugo watakupa maelezo ya kiasi cha kuchanganya.
Cha kuongezea kama upo mahali mvua zinanyesha sana na hauwezi kuianika nje. Pumba ukitaka ikae muda mrefu inatakiwa uitandaze ndani ya chumba kilicjhosakafiwa na uigeuza kila siku asubuhi na jioni.Manunuzi ya pumba yaendane na uhitaji kwa maana pumba haswa kutokana na kiasi cha unyevu inayokua nayo inawahi kuvunda (kutengeneza fangasi) na kuzalisha sumu kuvu kwa kitaalamu zinaitwa Mycotoxins.
Ufanyaje?
1. Hakikisha pumba inaanikwa kwenye turubai nje kwa ajili ya kupigwa na upepo na jua ili kupunguza kiasi cha unyevu. Unyevu mwingi husababisha pumba kuvunda haraka. Unyevu ukipungua pumba itakaa kwa muda mrefu
2. Usinunue pumba nyingi sana kuliko kiasi cha mahitaji ya kuku. Jitahidi kufanya makadirio ya manunuzi yako ukiangalia uhitaji. Pumba nyingi sana ni ngumu kuisimamia bila kutengeneza sumu kuvu
3. Kuna dawa za kuchanganyia kwenye pumba kupunguza sumu kuvu (mycotoxins) ambazo zinaitwa Mycotoxin binder. Unachanganya na pumba na zinashibiti kwa kiasi kikubwa sumu hiyo ya fangasi. Nenda duka la madawa ya mifugo watakupa maelezo ya kiasi cha kuchanganya.
Nashukuru kwa ushauri nitaufanyia kaziCha kuongezea kama upo mahali mvua zinanyesha sana na hauwezi kuianika nje. Pumba ukitaka ikae muda mrefu inatakiwa uitandaze ndani ya chumba kilicjhosakafiwa na uigeuza kila siku asubuhi na jioni.