Nimegraduate mining Engineering 2021 Udom, kozi ni nzuri sana shida ni limited number ya migodi mikubwa yani Large scale mines au Wizarani & Tume ya madini, ambazo ndizo zinalipa vizuri. Kikubwa ni kwamba kama huna ramani yoyote we omba Mungu tu pia uwe tayari kujitosa kwenye mashimo ya small scale mines ambayo ni rahisi kuingia lakini usalam wake ni mdogo sana kwa kuwa teknolojia yao ni ndogo unaweza ukapata pakuanzia ukagain yani usiwe muoga.
Pia kuna ishu za blasting ambazo unaweza ukafanya hata kwenye mine sites ambazo sio underground yani open pits au kwenye civil companies zinazofanya quarrying huwa wanaitaji mablaster etc
Basically itategemea unajiposition vipi ila ni sekta ambayo ina uhitaji mkubwa ila shida yake inahitaji uwekezaji mkubwa sana na unaoeleweka tofauti na hapo kazi ni nzito.