Naomba kujuzwa taratibu/masharti yanayoandikwa Guest House au Lodge

Naomba kujuzwa taratibu/masharti yanayoandikwa Guest House au Lodge

Kwa kuwa Babu yenu napenda mazoezi Wacha nifanye kabisa 🏋️🏋️🏋️
Babu,ugolo na mazoezi vunaingilianaje sasa😂😂😂hapo ndio unapofanyaga niahirishe safari ya kuja kukuona
 
Babu,ugolo na mazoezi vunaingilianaje sasa😂😂😂hapo ndio unapofanyaga niahirishe safari ya kuja kukuona
Hapana Mjukuu, unajua umri wetu huu wa Uzee, mazoezi ni muhimu sana hasa iwapo unategemea kupokea Wajukuu.

Maana nitalazimika kutembea kilomita nyingi kukupokea stendi 😜🏃🏃🏃
 
😅😅Mimi binti sayuni mjukuu wa maria magdalena ntaendaje nyumba za wageni angali mimi ni mkazi wa kudumi
Endelea hivyo hivyo binti Sayuni nataka kwenda kuchunguza kwanini kunajaaga hadi Yesu akazaliwa horini
 
Hongera sana mkuu, Muda kuisha kwa fedha ya mtu kwa siku hiyo ni muhimu sana pia idadi ya watu kwenye chumba kuna watu wanatoka mikoani wanataka kupanga chumba kimoja watu 5
Sawa mkuu.
Nitazingatia🙏
 
Jana na leo nimelala lodge mbili tofauti, Geita na Mwanza, na zote hazina hiyo karatasi ya masharti.

Maybe the trend ni kuachana nayo kabisa.
Pole kwa safari mkuu.
Kwa huku niliko naona bora kuwawekea tu
 
Mashaert yanaweza kuwa kwenye maeneo haya:
1.Bei
2.Muda wa kuingia & kuondoka:
3.Kuharibu, Kuvunja mali
4.Ufunguo kupotea:
5.Maegesho:
6.Marufuku Kuvuta Sigara,pombe
7.Makelele vyuumbani
 
Endelea hivyo hivyo binti Sayuni nataka kwenda kuchunguza kwanini kunajaaga hadi Yesu akazaliwa horini
Ha haaaaa haaa nyumba zilijaa wageni walioenda kwenye sensa na si vinginevyo!ila haya mambo yameanza zamani sana jamani
 
Taratibu na Masharti ya Nyumba za Wageni au Lodge

Taratibu na masharti ni kanuni ambazo hoteli, nyumba za wageni au lodge huweka ili kuhakikisha uendeshaji mzuri wa biashara yao na kulinda maslahi ya wateja na wafanyakazi. Masharti haya hutofautiana kulingana na ukubwa wa kituo, eneo na huduma zinazotolewa.

Hapa kuna baadhi ya taratibu na masharti ya kawaida ambayo unaweza kukutana nayo:

Uhifadhi:
Uhifadhi unaweza kufanywa kwa simu, barua pepe au mtandaoni.
Malipo ya awali yanaweza kuhitajika ili kuthibitisha uhifadhi.
Tarehe ya kufuta uhifadhi bila malipo inaweza kutofautiana.
Kuwasili na kuondoka:
Muda wa kuwasili na kuondoka kawaida huwekwa wazi.
Wageni wanatakiwa kuonyesha kitambulisho halali wakati wa kuwasili.
Malipo
Njia za malipo zinazokubalika hutajwa (fedha taslimu, kadi, nk).
Ushuru wa huduma na kodi zingine zinaweza kuongezwa kwenye bili.
Vitu vya kibinafsi:

Je, ungependa kujua kuhusu taratibu na masharti kwa aina fulani ya malazi, kama vile hoteli za kifahari au hosteli? Angalia hapa
 
Asante mkuu🙏
Napenda kujua ya Lodge mkuu🙏
 
As promised

1725638198106602709367271901942.jpg
 
Masharti na kanuni za nyumba ya kulala wageni (guesthouse) zinaweza kutofautiana kulingana na eneo na aina ya nyumba ya kulala wageni. Hata hivyo, ngoja nikupe mkuu baadhi ya masharti ya kawaida Ili mwana jamii forum aweze kulekebisha kwenye kasoro

1. Kitabu cha Wageni: Wageni wanatakiwa kujaza fomu ya usajili na kutoa vitambulisho vyao kwa ajili ya kumbukumbu.

2. Malipo: Malipo ya malazi yanaweza kuwa ya awali au wakati wa kuingia. Hakikisha unajua jinsi malipo yanavyofanyika.

3. Muda wa Kuingia na Kutoka: Kuna wakati maalum wa kuingia (check-in) na kutoka (check-out) ambao wageni wanatakiwa kufuata.

4. Kanuni za Kimya: Wageni wanatakiwa kuheshimu sheria za kimya ili kuepuka usumbufu kwa wengine.

5. Usalama: Wageni wanapaswa kufuata kanuni za usalama, kama vile kufunga milango na madirisha wakati wote, na kuacha funguo za vyumba kwa msimamizi wa nyumba ya kulala wageni wakati wa kuondoka.

6. Mikate na Vinywaji: Mara nyingi, nyumba ya kulala wageni itatoa au itakubali mikate na vinywaji vilivyochaguliwa, lakini wageni wanapaswa kuzingatia kanuni za matumizi ya vitu vya umma.

7. Vifaa vya Nyumba: Wageni wanatakiwa kutumia vifaa vya nyumba kwa uangalifu na kuzirudisha katika hali nzuri kama walivyozipata.

8. Madhara na Uharibifu: Wageni wanawajibika kwa madhara yoyote au uharibifu wanaoweza kusababisha kwenye mali ya nyumba ya kulala wageni.

9. Wakazi wa Kudumu: Mara nyingi, nyumba ya kulala wageni haitakubali wageni kuwa na makazi ya kudumu.

10. Wageni wa ziada: Wageni wanapaswa kuarifu mapema kuhusu wageni wa ziada na kulipa ada ya ziada kama inahitajika.
n
Sasa hizo ni baadhi ya kanuni zinazoweza kuwepo katika nyumba ya kulala wageni, lakini ni muhimu kwa wageni na waendeshaji wa nyumba ya kulala wageni kuwasiliana ili kuelewa masharti maalum.
 
Back
Top Bottom