Naomba kujuzwa taratibu za kubadili kazi Ualimu kuwa Afisa Lishe

Naomba kujuzwa taratibu za kubadili kazi Ualimu kuwa Afisa Lishe

nyahinga

Member
Joined
Dec 18, 2016
Posts
45
Reaction score
23
Habari JF,

Naomba kuuliza utaratibu wa kubadili kazi kutoka kuwa mwalimu na kuwa afisa lishe wa wilaya. Nimesoma BSc. In human Nutrition lakini pia nikasoma postgraduate diploma in education.

Kwa Sasa nafanya kazi kama mwalimu, Ila nataka kuhamia kwenye field ya mwanzo. Yaani nataka nifanye kazi Kama afisa lishe wa wilaya. Naomba kufafanuliwa kama inawezekana au la.

Shukrani sana.
 
Nawafahanu ma DNuO wengi tu na hata RNuO wa mikoa flan nimefanya nao sana kazi, ninaweza kukuunganisha nao ila sina uhakika kama wanaweza kukuingiza kwenye kada. labda uweke wazi unahitaji msaada gani tukusaidie.
 
Ongea na watu wa halmashauri hasa walio katika kada hiyo kama kuna gap andika barua omba recategorization.
 
Inawezekana sana. Ongea na DHRO wenu uandike barua ya kubadilisha muundo. Kama ikama haijatimia wanakubadilisha chapu.
 
Mimi nimesoma sheria ila nameajiriwa kama mwalimu ( PGDE) kwa hiyo mimi ni kama wewe , ila swali langu kwako umechunguza na umejiridhisha kuwa halmshauri ni sehemu sahihi kwako, kwa utafiti wangu halmshauri ni mahala pa kiboya zaidi , bora ubaki as mwalimu huku ukisubiri ajira za kuhamia kwenye mashirika na tasisi za serikali,
 
Waalimu ni kada nyonge Tanzania hii ni kutokana na walimu wengi kuwa vibaraka wa chama cha kijani..huku wakitumika kama TP.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nadhani sheria za utumishi zimeainisha kwenye swala la kuhama kada,itabidi uandike barua ukiambatanisha na vyeti vya taaluma yako uwasilishe utumishi watakaa na kama kutakuwepo na gepu basi utahamishwa.

NB: sio lazima ni uamuzi wao
 
Back
Top Bottom